''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, April 30, 2017

NGUVU YA KUTII

Mhubiri: Mr. Leadri Kinabo
Maandiko: Isaya 1:16-19

Ukianzia Isaya 1:3 utaona kwamba wana wa Israel walikuwa wamemuacha Bwana, kwahiyo hapa Mungu akawa anawaonya kumtii Mungu. Ndio unaweza ukawa uko vizuri sana kwenye vingi unakuja kanisani mara kwa mara, unasoma Neno na kuomba lakini je una mtii Mungu?, je unatii Neno lake?. 

Na baadhi ya watu wanazani kutoa sadaka ndio kitu muhimu sana kwamba Mungu anafurahia kila sadaka bila kuangalia hali yako ya rohoni, lakini si kweli Kutii Neno la Mungu au kile Mungu anachokuelekeza ndio cha muhimu zaidi. Ukiangalia Isaya 1:13 utaona wana wa Israel walikuwa wanamtolea Mungu sadaka nzuri na wakati walisha muacha Mungu, Mungu akakataa sadaka zao. Sadaka yako, fungu lako la kumi halina maana kama ukawa unalitoa bila kumtii Mungu, ukimuacha Mungu hata sadaka zako hatazikubali. 

Isaya 1:19 lakini ukiwa tayari na kutii Neno la Mungu, kumtii Mungu utakula mema ya nchi, kumbe ili ule mema ya nchi ni lazima umtii Mungu, lakini pia kumbe ina maana usipomtii Mungu hutakula mema ya nchi. Unajua kuna "kula nchi" na kuna "kula mema ya nchi" hivyo vitu viwili sio sawa. Lakini Mungu anatoa nafasi ya kujisafisha Isaya 1:16 acha dhambi unazofanya, dhambi zinakutenga mbali na Mungu, kubali kubadilika leo, ukibadilika na kumrudia Mungu utafanikiwa sana kwenye maisha yako.

No comments:

Post a Comment