''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, October 1, 2017

WEWE NI BALOZI WA YESU

Mhubiri: Mr. Elisha Suku
Maandiko: 2Wakorintho 5:17-20

Balozi ni mtu anayewakilisha nchi yake katika nchi nyingine, na anaheshimika, na analinda matakwa ya nchi yake. Sasa ukiokoka unakuwa balozi wa Kristo, wewe ni wa Kristo, unamuwakilisha Kristo popote ulipo kama ni kazini, kwenye biashara au shuleni. Kuna aina ya watu hawapati muda wa kuja kwenye mikutano ya injili au kanisani lakini kupitia wewe mtu uliyeokoka, kazini kwako, shuleni, au kwenye biashara, mtu yule anatakiwa apate habari za Kristo kutoka kwako, kutoka kwenye maisha yako ya kila siku.

Ukitaka kujua vizuri kuhusu nchi nyingine unamuuliza balozi wa ile nchi kwasababu yeye ndiye mwenye taarifa sahihi kuhusu nchi yake. Na sisi kama mabalozi wa Yesu Kristo hapa duniani inatakiwa tuwe tuna taarifa sahihi kuhusu Yesu yaani kuisoma na kuielewa Biblia vizuri na kuhusu wokovu, ili wale ambao hawajaokoka wapate taarifa sahihi za Yesu za wokovu kutoka kwetu.

Yawezekana bado hujajua Biblia sana lakini waambie watu nini Yesu alichokufanyia usiwaambie watu story wape ushuhuda wako kwamba Mungu amekutendea hili na hili hiyo inakuwa ina nguvu zaidi. Unajua nini Mungu alichokufanyia basi usipate shida wakati wa kushuhudia wewe sema tu Yesu alichokufanyia, tumebeba ujumbe wa UPATANISHO NA UNAWAKILISHA UFALME WA MUNGU. Usiache kusema na watu, watu wanakufa kwenye dhambi.

Sasa sisi kama mabolozi tumepewa kazi ya kupatanisha watu wengine na Yesu, ili wapate hiyo neema kama sisi tulivyopata. Tulikuwa tunaenenda kwenye giza tulizoea kufanya mambo ya gizani kufanya dhambi, lakini tukatolewa kwenye giza na kwenda kwenye nuru, na ukitembea kwenye mwanga inamaanisha unaona vizuri unaenda wapi.

Kama mabalozi wa Yesu hatutakiwi kuishi kwa viwango vya hapa duniani kwasababu sisi tunamuwakilisha Yesu, balozi anapokuwa kwenye nchi nyingine anaishi kwa utamaduni wa kwao sio wa ile nchi alipo, kwahiyo utamaduni wako sio wa hapa duniani usiishi kama mtu wa hapa duniani, ishi kama utamaduni wa Yesu. Pia balozi muda wake huwa unaisha, ukiisha anarudi kwenye nchi yake na wewe tambua kuwa muda wako ukifika utarudi kwa Kristo.

Sasa ili tuweze hayo yote ni lazima tuwe na mahusiano hai na Yesu muda wote, unakuwa na mawasiliano kwa njia ya kusoma Neno na Kuomba.

No comments:

Post a Comment