''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, March 31, 2019

KUJIKANA MWENYEWE

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Waebrania 12:1-13

Kujikana mwenyewe kunaenda na uvumilivu. Maisha yetu ya kiroho yanalinganishwa na mashindano ya kukimbia, tupo kwenye mbio, na kuwa kwenye mbio ni lazima uwe mvumilivu kadiri unavyokimbia unakutana na changamoto na vishawishi vingi. Kujikana mwenyewe kunahitaji bidii binafsi; mfano unapoamua kufunga na kuomba utaona ndo wakati ule unapewa ofa ya chakula sasa lazima ujikane kwa kukataa zile ofa, umeamua kufanya maombi basi usibadilishe mawazo kwasababu ya kitu fulani. Majaribu yatakuja shetani atakushawishi na kukunong'oneza, wale wakimbiaji huwa hawaangalia vitu ya njian bali huangalia ule mstari wa kumalizia. 


1Wakorntho 9:24-27, "Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. 25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. 26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; 27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa."

Wale wanaokimbia wanapitia mafunzo mazito na ili kushinda ni lazima waamue kweli kuwa makini na sisi vivyo hivyo, kama kweli unataka kwenda mbinguni lazima uwe makini na safari hii, safari hii/ mbio hizi hazihitaji michanganyo, ni lazima uamue kuacha dhambi zote na kumfuta Yesu.

Kama unataka kufika mbinguni ni lazima ukimbie mbio nzuri, usipokimbia vizuri huwezi fika mbinguni, mbinguni wataingia watakatifu tu. Ni lazima ujikaze na ujitahidi sana na kujiwekea adabu nzuri ili uweze kufika, utajiweka vizuri kwa kusoma Neno la Mungu na kuomba. Kila kitu kinacho kuzuia kusoma Neno la Mungu au kuomba viweke pembeni, dhambi inayokuzinga kwa upesi tamaa za mwili lazima uziweke pembeni!. Ni lazima ujikane mwenyewe na ubebe msalaba wako.

No comments:

Post a Comment