''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, July 14, 2019

GHARAMA YA KUWA MWANAFUNZI WA YESU KRISTO

Mhubiri: Mr. Frank Mwalongo
Maandiko: Luka 14:25-35

Yesu alikuwa anafuatwa na watu wengi sana, wengine ni kwasababu ya mikate waliyopewa, wengine kwasababu ya miujiza yake kwahiyo alikuwa anafutwa na watu wengi, sasa hapa Yesu akawarudia kuwageukia watu wale na kuwaambia sifa za wanafunzi anaowataka. 

Kuna gharama ya kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo, na hizo sifa kaziwek wazi kwenye Luka 14:26 "Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu." 

Hakumaanisha uwaachukie ndugu zako au wazazi hapana lakini Yesu Kristo awe namba moja kwako! kuliko vyote kuliko ndugu zako.  Kwa njia yoyote ile wasikuzuie kumtumikia ni bora uwakose, kipaombele cha kwanza kiwe ni Yesu Kristo. Ukujipenda wewe mwenyewe huwezi kuwa mwanafunz wa Yesu hayasemi ujichukie bali Yesu Kristo umuweke kipaombele namba moja kuliko vipaombele vyako binafsi. Yesu kwanza.

Luka 9:57-62 hapa kulikuwa na malumbano Yesu anawaita watu wawe wanafunzi wake lakini watu wale wanaanza kuweka vipaombele vyao kwanza kuliko kuliko kumfuata Yesu, kuwa mwanafunzi wake. Usiruhusu chochote kile kukuzuia usumtumikie Yesu Kristo.

Kama Utashindwa kuwa na vigezo vya kuwa mwanafunzi wa Yesu basi huwezi kuwa mwanafunzi wake, ni uwe mwanafunzi wake au usiwe mwanafunzi wake basi hakuna maelezo mengine hakuna kuwa mwanfunzi wa Yesu kidogo, ni uwe mwanafunzi au usiwe mwanafunzi wa Yesu, lazima uamue moja kutoka moyoni, Mungu hapendi michanganyo.

Luka 14:27 anavyosema kuhusu msalaba anamaanisha kujikana kwa hali sana. Kama hutaweza kubeba msalaba wako huwezi kuwa mwanafunzi wa Yesu, Inamaanisha kujikana mwenywe na kuwa tayari kwa ajili ya Yesu, uwe hata tayari kupoteza maisha yako, kuliko watu wakutenganishe na Yesu ni afadhali upoteze hata maisha yako.

Luka 14:33, uwe tayari hata kupoteza kila kitu kwasababu ya Yesu, hata kupoteza marafiki zako, rafiki mmoja tu anatosha kukurudisha nyuma/duniani, utaona kidogo kidogo utaanza kupunguza msimamo wako(u will start to compromise and slowly u will start to go back)

Hebu jiulize sasa Je wewe ni mwanafunzi wa Yesu? 
Jiulize Je unakidhi vigezo vya kuwa mwanafunzi wa Yesu? 
Omba msahamaha sasa kwa Mungu, kuwa tayari kuacha vyote, na kumuweka Mungu namba moja.

No comments:

Post a Comment