''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, July 28, 2019

UMOJA SIRI YA MAFANIKIO

Mhubiri: Mch. Kiongozi, Abdiel M. Mhini
Maandiko: Yohana 17:20-23, Efeso 4:13;4:3; 

Yohana 17:20-23
"20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi."

Yesu alipokaribia kupaa alifanya maombi, hakufanya maombi kwa ajili tu ya wanafunzi wake lakini aliwaombea mpaka watakaoamini injili ambao ndio mimi na wewe. Kati ya vitu alivyomuomba Baba yake ni kuwa atupe UMOJA, tuwe wamoja kama Yeye na Mungu Baba walivyo. Alijua umuhimu wa Umoja, umoja unaleta nguvu. Hauwezi kufanikiwa na kwenda mbali kama huna umoja na wenzako. Watu waliofanikiwa sana kiroho na kimwili utaona ni watu wenye umoja na ushirikiano sana na wengine. 


Sisi kama watu waliookoka, wote ni mwili wa Kristo, kila mtu ni kiungo kwa ajili ya mwenzake, kwahiyo inatupasa kuwa na umoja kati yetu. Tukiwa na Umoja tunapata nguvu ya kufanya kazi ya Mungu kubwa zaidi kuliko ukiwa mwenyewe. 

Efeso 4:13. Efeso 4:3 jitahidi sana kuwa na umoja wa kiroho, sisi kama watumishi wa Mungu tuwe na umoja kaatika Roho tuweze kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu.

No comments:

Post a Comment