''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, March 24, 2013

UJUMBE WA LEO: UFAHAMU JUU YA MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO
-----------------------------------------------------------------------------------
MAANDIKO: Mathayo 25:1-13
MHUBIRI: Mch. MHINI
--------------------------- 

Tunaishi wakati ambao uraia wetu wa hapa duniani unaelekea ukingoni. Yesu anakuja kuchukua kanisa lake, kila kitu chenye mwanzo kina mwisho ni kweli tumeshazoea kusikia siku za mwisho na inawezekana unachukulia ni kitu cha kawaida lakini hii ni kama mchezo wa mpira wa miguu baada ya dakika 90 refa akipiga pilimbi ya kumaliza, mpira unaisha haijalishi umepata hujapata goli hata moja au umepata magoli mpira utaisha. Kipindi tulichonacho sasa ni kipindi cha mwisho zaidi ya mwisho Yesu anarudi muda wowote kwanzia sasa na akirudi haitajalisha umetubu au hujatubu historia yamaisha yako itakuwa imeishia hapo na utatakiwa kusimama mbele ya kiti cha hukumu, ni heri leo uamue kuishi maisha matakatifu yasiyo na mawaa.

Neno la leo linaonyesha wenye busara watano walio weka mafuta ya akiba na wapumbavu watano ambao hawakuweka akiba ya mafuta. Je! Una mafuta ya akiba? Mafuta ni uaminifu, Je! Umeambatana na Roho Mtakatifu?

 Ishara zote za siku za mwisho zinaonekana wazi sasa, kama sunami, vimbunga vya hurricanes, njaa, vita katika nchi mbalimbali, pia roho chafu kutoka kuzimu zimesambaa sana uovu umekuwa nje nje. Mathayo 24:7-14,36,42,44 inaoshenya ishara mbalimbali na hayo yote yametokea sasa ni kwa kiasi gani umejiandaa?

No comments:

Post a Comment