''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, April 14, 2013

JUMAPILI MWENGE TAG!!UJUMBE WA LEO: LIONDOE JIWE
----------------------------------------
MHUBIRI: Mwinjilisti Isaya Masokola
MAANDIKO: Yohana 11:38-44
--------------------------------------- 


 Ni nini kinacho kusumbua leo? Ni kitu gani kinakuzuia leo? Kitu gani kinakurudisha nyuma kiroho na kinakufanya usitende mapenzi ya Mungu?, Liondoe jiwe linalo kusonga katika maisha yako. Yesu aliwaambia watu wa nyumbani kwa Martha kwamba Liondoe jiwe. Jiwe linaweza kuwa ni kazi yako, dini yako, au desturi yako uliyojiwekea katika maisha yako. Ondoa jiwe katika maisha yako.

Ukiondoa jiwe utafanikiwa na maisha yako hayatakuwa kama mwanzo. Ndugu nakusihi ondoa jiwe na utafanikiwa, Hautakuwa tena mtu wa kawaida , maisha yako yatabadilika. Kubali leo kuondoa jiwe.

Baada ya kuondoa jiwe mwamini Yesu. Mstari wa 40, Yesu aliwauliza, Mimi sikuwaambia ya kwamba ukiamini utaona Utukufu wa Mungu?. Watu wale walisikia Neno la Mungu lakini hawakuamini. Ndugu yangu siku ya leo amua kwa kumaanisha kuamini Yesu anacho sema na kumwamini Yesu mwenyewe. Watu wengi siku za leo wamekuwa wakishika sana maandiko lakini sio Neno La Mungu.

Kuna utofauti mkubwa kati ya Maandiko na Neno la Mungu, Neno la Mungu linaponya lakini maandiko hayaponyi, maandiko hayabadilishi maisha yamtu lakini Neno la Mungu linabadilisha maisha, Ukishika maandiko na kukariri sana mistari hiyo haitakubadilisha lakini Ukishika sana Neno la Mungu ukilijaza kwa wingi moyoni mwako maisha yako yatabadilika. Wengi sasa wanasoma sana Biblia lakini bado ni waongo, wanasema wenzao, wazinzi ni kwasababu wameshikika maandiko na sio Neno la Mungu. Ndugu yangu amua leo kushika Neno la Mungu na kuliamini, utaona maisha yako yakibadilika hata majirani zako marafiki zako watasema kweli unaye Mungu. Usipo fanya hivyo hutaweza kuishi maisha matakatifu.

Ukiamini Neno la Mungu utaona Utukufu wa Mungu, mapepo hayatakusogelea, magonjwa yatatoka. Amua leo kuwa na Yesu kwa kumaanisha na kuishi naye kisawasawa. Hebu fika mahali ujivunie kuwa na Yesu maishani mwako, watu wanaokuzunguka waone kweli una Yesu. 


 Lazaro alipotoka kule kaburini alikuwa bado amefungwa na wakati ule alikuwa hawezi kufanya kitu mpaka alipofunguliwa zile sanda, Watu wengi siku za leo wameokoka sawa lakini bado wamefungwa na shida nyingi kama magonjwa, madeni nk. Lakini kumbuka Yesu yupo leo kwa ajili yako, mkabidhi shida yako leo. 


                                                            Lazaro akifunguliwa..

Lazaro akiondolewa vifungo vyoteNo comments:

Post a Comment