''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, April 22, 2013

IBADA YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU

MAANDIKO: Yoeli 2:28-29, Matendo 1:4-8, Matendo 2:1-4
MHUBIRI: MCH. MHINI
----------------------------------------------------------------
Habari ya Roho Mtakatifu ilianza kutabiriwa tangu kipindi cha Yoel, ya kwamba roho itamimininwa kwa wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono. Na Bwana akamalizia na kusema ataimimina Roho yake juu ya watumishi wake waume kwa wake.
 
Nguvu za Roho Mtakatifu zilianza kuwashukia mitume siku ile ya pentekoste, ni siku ya 50 ya mavuno iliyokuwa ikisherehekewa katika agano na kale. Mitume walijazwa nguvu na wakaanza kusema kwa lugha nyingine. 

Roho Mtakatifu ni Nguvu na inatakiwa iendelee ndani yako muda wote, ikipungua mrudia Mungu rekebisha pale ulipodondoka. Tamani sana kuwa na Roho Mtakatifu kwasababu Roho Mtakatifu ndiye atakaye kuwezesha kushuhudia wengine bila aibu, kuponya na kufanya kazi nyingine za Mungu.

Kunena kwa lugha ni ishara ya nje inayodhihirisha kujazwa na Nguvu za Roho Mtakatifu. lakini wapo watu wanao igiza kunena, Hakikisha ndugu yangu unampata Roho Mtakatifu wa Kweli na sio wa kuigiza kunena. Nguvu ya Roho Mtakatifu ikipotea ndani mwako maadui wako wataingia, unakuwa umempa nafasi shatani.














 

No comments:

Post a Comment