''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, May 12, 2013

FUNGU LA KUMI(TITHE)

MAANDIKO: Mwanzo 14:18-20
MHUBIRI: Mch. Mhini

Fungu la kumi ni asilimia kumi(10%) ya mapato yako yote, mapato hayo yanaweza kuwa ni mshahara wako,mapato kutoka kwenye biashara yako au pesa uliyopewa na mtu kwaajili ya matumizi yako. Kila pesa unayopata unatakiwa utoe fungu la kumi, Mfano ukipata elfu kumi(10,000) asilimia kumi ya ni elfu moja, kwahiyo utatakiwa utoe hiyo elfu moja.

Katika maandiko hayo tunamuona Abramu akimtolea Mungu fungu la kumi la vitu vyake vyote. Zamani, watu walikuwa wanatoa fungu la kumi ili liwasaidie wale walawi waliokuwa wakitumika katika nyumba ya Bwana, vivyo hivyo hata leo. Fungu la kumi kwa sasa linatumika sehemu nyingi kama kulipia bili za umeme na maji ya kanisa n.k, pia zinatumika kuwategemeza watumishi wa Mungu na familia zao. Fahamu kwanzia leo kwamba kuwatunza watumishi wa Mungu na familia zao ni jukumu lako wewe.

Usiwe mgumu au mzito kutoa fungu la kumi kwasababu hata hizo pesa au mali ulizonazo sio zako ni za Mungu, wewe hukuja na kitu duniani na hutaondoka na kitu dunia, katika Ayubu 1:21, Ayubu alilitambua hilo. Kwahiyo pesa, nyumba, magari na mali zote ulizonazo ni Mungu amekupa tu kwa neema, basi amua leo kumpa asilimia kumi. Mungu amekupa kazi inayokupa mshahara flani au ni biashara inayokupa mapato, sasa Mungu anahijati asilimia kumi tu ya mapato hayo. Usipende mali mpaka ukamsahau aliyekupa hizo mali, aliyekupa afya, uwezo na nguvu za kutafuta hizo mali. Ukipenda mali kuliko kumpenda Mungu hiyo itakuwa ni ibada ya sanamu Wakolosai 3:5.

Usipotoa fungu la kumi utakuwa umeweka mali zako katika mfuko uliotoboka yaani pesa yako itaisha ghafla na kwa njia za ajabu, mara utashangaa mwenzako flani anaumwa utatakiwa utoe hela au matatizo mengine tu yatatokea na kuimaliza ile pesa ambayo hukuitolea fungu la kumi. unapoteza mali zako kwasababu umelaaniwa Malaki 3:8-9. Tambua leo, kwamba kama hutoi fungu la kumi umelaaniwa. Na kuna uwezekano unashiriki Meza ya Bwana alafu hutoi fungu la kumi.

Mali zako zinapotea kwasababu umepoteza Ulinzi wa Mungu. Ukitoa fungu la kumi Mungu anamzuia yule muharibifu. Usiwe na visababu vya kutokutoa fungu la kumi. Usipotoa ni sawa na kufukia talanta yako Mathayo 25:24-25  

No comments:

Post a Comment