''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, June 9, 2013

ROHO MTAKATIFU NDIO UFUNGUO WA UAMSHO

MAANDIKO: Wakolosai 2:6-7, Wakolosai 3:1-7
MHUBIRI: Mch. A.M.Mhini
Tuliambiwa tukae ndani ya Roho Mtakatifu tangu siku ya kwanza tuliookoka lakini hali hii imekuwa ikipungua polepole ndani ya makanisa yetu, Wastu wengi sasa wamekuwa hawaoni umuhimu wa kuaka ndani ya Roho Mtakatifu na wengi wao wamempoteza kabisa kwasababu ya kuipenda dunia na mambo yake zaidi ya kumpenda Mungu.

Inawezekana kabisa ulikuwa mzuri katika maombi, ulikuwa sio mzito kufunga na kuomba, ulikuwa unakuja sana katika mkesha, lakini sasa umepunguza au umeacha kabisa. Kama una hali hiyo jua kwamba kuna kitu cha muhimu kimepungua ndani mwako nacho ni Roho Mtakatifu, Umemuacha Roho Mtakatifu. Huna hamu tena ya kusoma Biblia/Neno la Mungu, huna hamu tena ya kuomba ni kwasababu Roho Mtakatifu hayupo ndani mwako.

Ni kweli ulijazwa Roho Mtakatifu siku zilizopita lakini sasa hayupo hai ndani mwako ameondoka ndani mwako ni kwasababu wewe ndie uliyemuacha, matendo yako ndio yaliyo mfukuza ndani mwako. Umekuwa mzito kuja kwenye ibada za katikati ya wiki, umekuwa huna mguso tena wa kutii matangazo yanayotangazwa madhabahuni.

Mara ngapi umeambiwa uje ibada za katikati ya wiki hujaja? Kwanini?, Rooho Mtakatifu ameondoka ndani mwako. Sahivi ukifanya dhambi roho haikusuti tena unajisikia kawaida kabisa, Vitu visivyo vya kawaida unaviona kawaida ni kwasababu huna Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndicho chombo muhimu katika wokovu

No comments:

Post a Comment