''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, December 29, 2013

MAAGIZO YA BWANA KWA KANISA

Mhubiri: Mchungaji Kiongozi Mhini
Maandiko: Matendo 2:42-47 

Moja ya maagizo ni Meza ya Bwana au Ushirika Mtakatifu. Tunapaswa kuangalia mwanzo wa kanisa na baada ya pentekoste walishiriki vipi Meza ya Bwana. Awali ya yote ya maagizo ya kanisa tuliyoagizwa na Yesu mwenyewe hayapaswi kusahauliwa, kwa mujibu wa Meza ya Bwana soma mathayo 26:26-30, hapa tunaona Bwana alihuzunishwa sana moyono mwake kwasababu alikuwa anajua kinachoenda kutokea kwahiyo akawakusanya wanafunzi wake katika meza akashukuru akaugawa mkate kwa wanafuzi wake akasema twaeni mle huu ndio mwili wangu kwahiyo mkate ni alama ya mwili wa Yesu. Unapokula mkate tambua unakula mwili wa Yesu, Yesu alijua mwili wake utaenda kutundikwa msalabani lakini aliona kabla ya muda ule haujafika ngoja aache alama ya mwili wake na huo ndio mkate uliomegwa na divai ni alama ya damu yake aliyomwaga pale msalabani. 

Ni muhimu kushiriki Meza ya Bwana kwasababu ni sadaka yake kwa ajili ya ukombozi wa wanadamu. Kwahiyo unaposhiriki Meza ya Bwana usichukulie kama ni kitu cha kawaida na kushiriki Meza ya Bwana ni amri,  kama wewe umeokolewa unapaswa kushiriki Meza ya Bwana. Kuna wengine muda wa kushirikki wanatoka nje ya kanisa sasa inashangaza ni kwanni unatoka nje na unaacha kushiriki Meza ya Bwana. Leo nakukumbusha kwamba kushiriki Meza ya Bwana ni amri kutoka kwa Bwana. 


No comments:

Post a Comment