''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Thursday, December 26, 2013

TANGAZO KUU TOKA MBINGUNI

Mhubiri: Mrs. Masembo 
Maandiko: Luka 2:8-11 

Mariam bikira alipata tangazo kutoka mbinguni, lilikuwa tangazo kuu na la kushtusha lakini mariam ilibidi akubali. Pia herode aliposikia kuna mfalme amezaliwa na kwamba ilitabirika tangia miaka mingi kwamba Mfalme huyo atakuja, naye herode akatoa tangazo lake baya, yawezekana umesikia matangazo mengi lakini leo kuna tangazo kuu kutoka mbinguni linasema hivi kuna habari njema maana kwa ajili yako mtoto amezaliwa (yoh 1:12-13).

 Tumepewa mtoto mwanamume, katika kitabu cha Isaya, maana kwajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa Mtoto wa kiume na uweza wa  Kifalme upo mamegani mwake. Hata kama wanaseme wewe ni mgonjwa sana lakini sikiliza tangazo kutoka mbinguni kwamba mtoto amezaliwa kwaajili yetu na tumepewa mtoto huyo wa kiume, na majina yake ni mshauri wa ajabu, zaburi 32:8, mtoto tuliopewa sio wa kawaida bali ni mshauri wa ajabu hata kwenye kazi yako au biashara yako yawezekana imefika mahali ambapo haiendi vizuri lakini Yesu ni mshauri wa ajabu kwahiyo mwambie katika hili Yesu nishauri, mwambie Yesu hujazaliwa kwa bahati mbaya muulize unataka mwaka unaokuja 2014 nikutumikieje. Jina lingine ni Mungu mwenye Nguvu aliye shinda mauti sasa kama alishinda nguvu za mauti ni kitu gani asichokiweza?. Jina lingine ni Baba wa milele, baba wa hapa duniani inafika kipindi wanakuacha wanaweza kufa au anaweza kukuvunja moyo sana lakini yuko Baba wa milele asiyebadilika kamwe. Akasema tena yeye vitu vyote ni vyake, baba wa milele hatakuacha. Yawezekana uko bado hujaokoka lakini huyu Yesu tunayemkumbuka leo kuzaliwa kwake anaweza kukuokoa. Jina jingine ni Mfalme wa amani, kuna muda unakosa amani, yawezekana unavaa vizuri au una hali nzuri sana lakini huna amani lakini Yesu yupo kwajili yako, Isaya 61:1-3, KWA AJILI YAKO YESU KRISTO MWOKOZI AMEZALIWA, basi mng'ang'anie Yesu. Yesu alisema amekuja kuwatangazia mateka uhuru wao, inawezekana ukipiga hatua hivi hauendi shetani amekushikilia lakini Yesu ametangaza uhuru wako. 

Pia alitanga mwaka uliokubalika, yawezekana umezunguka vya kutosha mahali ulipo lakini habari niliyonayo ni hii Yesu amekuja kukuweka huru. Yesu hataisahau bidii yako, sasa geuka mwangalie Yesu mwambie umetengaza mwenyewe mwaka uliokubalika kwahiyo atengeneze mazingira yako, inawezekana una vilio vingi vya watoto wetu au maofisini au mashuleni, lakini basi yale machozi yako mwambie Yesu niko mahali hapa mwaka 2014 nisiingie hivi nilivyo. Yesu ametangaza mambo mengi kinachohitajika ni wewe tu kutengeneza maisha yako vizuri na umkaribishe Yesu ndani mwako.

MWAMBIE BWANA YESU ULIOZALIWA LEO KWA AJILI YANGU NATAKA KUINULIWA, NIMETESEKA VYA KUTOSHA NA UMEZALIWA KWA AJILI YANGU NATAKA LEO KUINULIWA KWANGU.NAOMBA UNISAIDIE KWENYE MAMBO YANGU.

No comments:

Post a Comment