''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, March 30, 2014


UJUMBE: MALENGO MATANO ALIYOKUSUDIA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO
MHUBIRI: Mr. Benard Okech
   
1. Ulikusudiwa kwa ajili ya Furaha ya Mungu (KUABUDU) Isaya 61:3-5, Ufunuo 4:11
Mungu aliumba viti vyote na kwa mapenzi yake vilikuwako, Mungu alitaka uwe hai na kufika kwako duniani na kapata burudisho.

2. Uliumbwa kwa ajili ya jamii ya Mungu, Warumi 14:19.
Mungu amekuumba ili ujaze jamii yake kwa kuwa mwaminifu, mnyenyekevu, mwenye adabu na mtu asiye toa siri za wengine.

     3. Uliumbwa ili ufanane na Kristo, Mwanzo 1:26-27, Warumi 8:29
Katika uumbaji woote wa Mungu ni binadamu tu ndiye aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mungu alituumba na kutuwekea roho ndani mwetu kama Yeye alivyokuwa Roho,  pia akatupa uwezo wa kufikiri na kutatua matatizo mbalimbali, ametupa busara, uwezo wa kupenda na kupenda, na wenye busara na uwezo wa kujua mema na mabaya.

4. Uliumbwa ili kumtumikia Kristo,1 Petro 4:10
Kila uwezo ulionao unaweza kuutumia kwa ajili ya Utukufu wa Mungu. Kila mtu amepewa uwezo flani na Mungu na pia una uzoefu mbalimbali kutokana na maisha uliyopitia, inawezekana ni uzoefu uliopata kutokana na jamii unayoishi nayo, au elmu uliyonayo, kazi uliyonayo au hata kutokana na karama uliyonayo. Uwezo au uzoefu huo unaweza kuutumia kuwahubiri watu waliopitia katika hali hizo.

5. Uliumbwa kwa ajili ya Utume
Utume wako ni muendelezo wa utume wa Yesu hapa duniani.  Unaweza kutumia shuhuda zako mbalimbali kushuhudia watu wanaopita katika hali kama hizo, mfano unaweza ukamuelezea mtu jinsi Yesu alivyokuokoa naye akashawishika kuokoka.

No comments:

Post a Comment