''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, May 11, 2014

ISHI KAMA MTOTO WA MUNGU

Maandiko: Yeremia 51:11-14,Galatia 4:3-7
Mhubiri: Immaculate from Global Harvest college. 

Neno la leo lina tukumbusha baraka tulizonazo kama watoto wa Mungu na hizo hatukustahili bali tulipata kwa neema, Mungu ametupa fursa ya kuja nyumbani kwake na kwa kifo chake tulipata kuwa wana. Biblia inasema tumepewa uwezo wa kuwa wana, Warumi 8:12-17, Galatia 4:3-7, ishi kama mwana na sio kama yatima sisi kama wana,  kuna vitu viwili vilivyotokea baada ya kumpokea Yesu, 
1. Tulifanyika upya, 
2.Tulifanywa wana tuliingizwa katika familia ya Mungu so tulipewa hadhi ya watoto ambao wanaweza kurithi, tumeondolewa katka utumwa tumekuwa wana, na ukigundua hilo tutaishi kama watoto wa Mungu. 
 Tulipewa uwezo wa kuwa wana wakubwa wanaoweza kurithi. 

Katika Galatia inaongelea hili vizuri, inaongelea sheria ukilinganisha na neema, inalinganisha siku wana wa israel walizoishi chini ya sheria na siku walizotakiwa kuishi kwa imani katika Yesu, hili liliongelewa kwasababu katika wakati wa paulo kulikuwa na watu waliokuwa wanataka kuishi chini ya sheria wakati washampokea Yesu, wayahudi waliendelea kuishi chini ya sheria na kutaka kuwafanya mataifa waliompokea Yesu kuishi chini ya sheria. Pia akasema kuhusu watu waliookoka wanaoishi kwa kufuata mambo ya dunia hii kwamba hao ni wachanga katika imani, haijalishi una miaka mingapi katika wokovu lakini kama bado unaishi kwa kufuata namna ya dunia hii wewe bado ni mchanga. 

No comments:

Post a Comment