''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, July 6, 2014

THAMANI YA WOKOVU

Mhubiri: Mr. Frank Mwalongo

Maandiko: Mathayo 19:21-30Tumeokolewa ndio  lakini dhamani  ya wokovu wetu ni nini? Kwahiyo tukijua dhamani ya wokovu wetu nini  hiyo itafanya tuulinde zaidi kama una dhamani ndogo tutakuwa hatuna haja ya kuulinda lakini kama una dhamani kubwa lazima tuutunze kwa gharama yoyote.
Mathayo 19:21-30, wakati huu Yesu alitaka wanafunzi wake wajue dhamani ya wokovu wao, kwahiyo akaanza kuongelea maswala ya yule tajiri, Yule tajiri aliyekuwa ana kila kitu na aliyesema amefanya kila kitu kwa ajili ya kuurithi ufalme wa Mungu, umefanya vitu vingi ndio lakini nenda kauze mali zako zote halafu unifwate, kwasababu Yesu alijua Yule tajiri alikuwa anategemea ule utajiri wake alikuwa anaabudu utajiri wake, kwahiyo akawa ana mwambia umefanya kila kitu ndio na kwasababu wewe ni tajiri ili unifwate kauze mali zako zote na ugawie masikini kisha badae unifuate. 

Yesu alipokuwa anaongelea swala hilo kwa wanafunzi wake wanafunzi walishangaa alipomaliza kuongea na yule tajiri akaja kwa wanafunzi wake akawaambia wanafunzi wangu ni ngumu sana kwa tajiri kuingia mbinguni na ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano ukilinganisha na tajiri kwenda mbinguni,  na Yesu alisema hivyo ni kwasababu ya matajiri kuabudu utajiri wao, Yesu hasemi kuwa hatufai kuwa matajiri lakini ukiwa tajiri na unaabudu utajiri wako nenda kauze mali zako ili uweze kumuabudu Yesu ndomana Yesu alisema hivyo. Alitaka wanafunzi wake wajue dhamani ya wokovu, inafaa ujue uwe tayari hata kuuza mali zako zote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 

Yesu aliwaambia hivyo wanafunzi wake kama kuwapa changamoto na akawaangalia machoni kwasababu alijua hata wanafunzi wake watakuwa na hiyo shida na wanafunzi wake wakashangazwa sana na wamafunzi wake wakajibu kwendana na mtazamo ule kwamba  wauze mali zao alafu wamfuate Yesu, sasa wakamwambia Yesu tumeacha mali zetu  kazi zetu Je! Sisi tutapata nini? Sisi tutapata nini Yesu? Na Yesu alikuwa anataka waulize hilo swali, na anahitaji wewe uulize hilo swali kwamba umeacha kila kitu je utapata nini na jibu la hilo swali ni kuhusu udhamani wa wokovu wetu, tumeokolewa ndio lakini tunapata nini, na Yesu akawaambia wanafunzi wangu nawaambia ukweli nitakapoketi kule kwenye kiti cha Enzi kuhukumu makabila 12 nyie mtakaa nami, na hilo ndio lilikuwa jibu. Kama umeokolewa na unaishi maisha ya utakatifu Yesu anakwambia atakapokaa katika kiti cha Enzi utakaa pamoja na Yesu. Ukisoma kitabu cha Yohana 3:18, 5:24, Yesu hakuja kuhukumu ulimwengu bali kuokoa na wale walio okolewa hawata hukumiwa kwasababu tayari wana uzima wa milele lakini wale waliomkataa wamekwisha kuhukumiwa kwasababu wameukataa wokovu. Pia akawaambia wanafunzi wake chochote walichokiacha na kumfuata Yesu watazidishiwa mara 100. Kwahiyo chochote ulicho acha kwa ajili ya Yesu utapata mara mia lakini si hicho tu bali na Uzima wa milele.

Mr. Frank Mwalongo akiwa anahubiri

No comments:

Post a Comment