''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, October 12, 2014

YESU NI JIBU

Mhubiri: PASTOR CHESTER WHISONANT(Kutoka Atlanta,Marekani)
Maandiko: Mathayo 15:21-28

Inawezekana unapitia katika hali ngumu au inawezekana shetani anashambulia familia yako inawezekana umepoteza kazi, inawezekana umepoteza mahusioano/ndoa, inawezekana umepoteza mali zako lakini haijalishi uko mazingira gani Yesu ndiye jibu. Wakristo huwa tunapata shida lakini katika kristo, Yesu hakusema kwamba maisha yetu yatakuwa ya raha tu, na kama hutaabiki katika Kristo inawezekana humfuati kisawasawa, Wewe ni lazima upate matatizo lakini cha muhimu au cha kuzingatia ni nini unafanya katika hayo matatizo/mateso.

Yawezekana umepanga nyumba na mwenye nyumba anakusumbua sana lakini kumbuka bado Yesu ni jibu atakupa nyumba yako. Haijalishi unapitia kwenye hali gani Yesu ni jibu.

Habari tulio soma leo ni kuhusu mwanamke, mwanamke huyu alikuwa na shida, alikuwa na matatizo mawili katika maisha yake. Kwanza hakuwa myahudi alikuwa mpagani, na wakati ule waliamini kuwa kama wewe sio myahudi huwezi kumuona Yesu kwasababu Yesu alikuwa myahudi, na myahudi na mtu asiye myahudi haikuruhusiwa kuongea pamoja. Na shida yake ya pili ni binti yake alipagawa na mapepo. 

Alifikia mahali katika maisha yake ambapo asingeweza kuendelea tena, na alifika mahali pa kuchanganyikiwa kwasababu ya shida anazopitia, sasa nataka nikuulize swali, je wakati mwingine unafikia wakati kama huo? Je huwa unafika wakati unaona kama hakuna jibu? Je unamewahi kufika mahali unaona hakuna msaada wowote? lakini siku zote kuna msaada na msaada huo ni Yesu Kristo. Wewe kama unasoma ujumbe huu, husomi kwa bahati mbaya bali ni Mungu mwenyewe ndiye aliyefanya uupate ujumbe huu, Mungu anataka kubadilisha maisha yako. Na unaweza ukamuomba Yesu akusamehe dhambi zako.

KANUNI 4 ZA KUFUATA UKIWA KATIKA MATATIZO
1.  Mgeukia Yesu
2. Yesu atabadilisha maisha yako wakati Yeye akiwa tayari na sio wewe ukiwa tayari, Mungu anaweza kuruhusu uteseke muda kwa muda flani ili ujifunze kitu katika tatizo hilo.
3. Usikate tamaa, Yule mwanamke hakukata tamaa
4. Imani kubwa huleta matokeo makubwa





No comments:

Post a Comment