''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, November 9, 2014

KUTAMKA NENO LA MUNGU UNAPOPITA KWENYE MATESO/SHIDA

Mhubiri: Mch. Amon Nyimbi Kutoka Kibwegele  
Maandiko: Ezekiel 37:1-14, Ezekiel 3:1-3 

Kutamka Neno la Mungu wakati wa shida wakati wa majaribu, ziko nyakati nyingine watu tuliookoka tunapitia nyakati za kujiliwa, ziko nyakati tunapita tunakutana na magumu. Mungu anapo muonyesha Ezekiel maono anamchukua akampeleka kwenye bonde ambalo lilikuwa limejaa mifupa tena mifupa mikavu sana iliyokuwa imetawanyika, Mungu alamuuliza Ezekiel mifupa hii yaweza kuishi? Ezekiel akasema Bwana Wewe wajua, Mungu akamwambia tena Ezekiel itabirie hii mifupa ili iweze kuishi naye Ezekiel akafanya hivyo. 

MAMBO 5 AMBAYO EZEKIEL ALIYAONA KWENYE  YALE MAONO 
1.Mifupa iliyo tawanyika na alivyoitabirika mifupa ikaanza kusogeleana mfupa kwa mfupa mwingine na ikaungana 
2.  Mungu akatokeza mishipa juu ya ile mifupa, hata kama una tatizo la mifupa yuko Yesu anayeweza kukuponya kila tatizo 
3. Nyama ikatokea juu ya ile mifupa 
4. Ngozi ikatokea juu ya ile nyama ya mifupa 
5. Ezekiel aliitabiria pumzi ndani ya ile mifupa nayo ikapata kuishi tena, na pumzi hiyo kwa sasa ni Neno la Mungu

Yawezekana unahangaika unatafuta, umepoteza haki unatishika na majina makubwa ya nabii au mitume lakini nataka nikwambie yuko Yesu anayeponya, Yuko Yesu ambaye anafungua vifungo kama utatembea katika Neno la Mungu. Unajua shida kubwa sasa ni kwamba hujatembea katika Neno na Mungu na hiyo inafanya uzunguke kuombewa katika makanisa mbalimbali lakini bila kupona, lakini nataka nikuambie ukiwa na Neno la Bwana hautaangaika wala hautazunguka kwasababu yuko Yesu ambaye unatembea nae amekuzunguka na wakati mwingine wanadamu wanaweza kukuacha lakini Yesu hawezi kukuacha, hakuna sababu ya kupata shida yuko Mwanaume anayefanya miujiza yuko Yesu anayefanya mambo makubwa. Watu wengi sahvi hawatembei ndani ya Neno la Mungu na ndomana hata siku za ibada za katikati hawahudhurii na wengine ikifika sunday school anaondoka ni kwasababu hawataki Neno la Mungu bali wanataka kuombewa tu na wengine wamekuwa wazinzi na wezi ndani ya makanisa, nataka nikwambie kuna mambo mengine hayahitaji kuombewa yanahitaji kutembea kwenye misingi ya Neno, unahitaji kutembea na Yesu na mambo makubwa yatafanyika.

MAMBO 4 YA MSINGI SANA 
  1. Tembea katika agano lako na Mungu, hicho ndicho kitu kitakacho kusaidia Zaburi 89:34-35, unajua baada ya kuokoka, baada ya kumwamini Yesu tuliweka mapatano, tuliweka agano na Mungu sasa kama tuliweka agano na Mungu lazima tutembee katika agano hilo.ukitembea katika agano la Mungu mambo makubwa yatafanyika katika maisha yako
  2. Ondoa vinyago, unahitaji kuondoa vinyago ulivyonavyo Mwanzo 31:33-35 
  3. Lazima tushikamane na tuwe na mfalme mmoja tusiwadharau watumishi wa Mungu
  4. Lazima ujitabirie Neno la Bwana Mathayo 8:5-15

No comments:

Post a Comment