''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, February 8, 2015

UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Matendo 1:4-5,8

Bwana Yesu tangu siku za mateso yake alisema sitawaacha ukiwa bali nitawaletea Msaidizi/Roho Mtakatifu. Chanzo cha nguvu ya utendaji ni Roho Mtakatifu, na hitaji kubwa sana la kanisa ni Roho Mtakatifu huyo anapokosekana halina mamlaka, huyo anapokosekana kanisa halina ukristo, huyo anapokosekana kanisa halina mwelekeo wa kweli, lakini Roho Mtakatifu akiwepo Roho Mtakatifu akitawala kanisa litakuwa na Nguvu, Mamlaka na Uweza Mkuu na kanisa ni wewe. Kama wewe na mimi sote tukijaa kiu na njaa ya Roho Mtakatifu utaona matendo makuu ya Mungu yakitendeka.
 
Lakini Je, Roho Mtakatifu ni kwa kiasi gani umempa nafasi katika moyo wako? kwasababu Bwana Yesu alisema wazi wazi kwamba hii ni ahadi kwa kanisa wakati anaondoka kwamba mtapokea Nguvu (Matendo 1:8) kwahiyo kabla ya kujazwa Nguvu za Roho Mtakatifu nguvu inakuwa haipo unaweza ukawa na hisia na misisimuko lakini nguvu inakuwa haipo mpaka utakapojazwa Roho Mtakatifu. Na hii Nguvu ya Roho Mtakatifu ipo na itaendelea kuwepo mpaka Yesu atakaporudi ni utayari wako tu kuipokea.

No comments:

Post a Comment