''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, February 1, 2015

SIMAMA KATIKA KWELI YA NENO LA MUNGU

Mhubiri: Mch Kiongozi ABdiel Mhini
Maandiko: Isaya 55:10-11,Luka 4:4,Waebrania 4:12-13,Ezekiel 3:1-6

 Neno la Mungu ni Neno lenye Baraka, ni Neno lenye Nguvu, ni Neno lenye Mamlaka, ni Neno lenye Uweza. Neno la Mungu kupitia nabii Isaya kama mvua ishukavyo kutoka juu hairudi huko bila kutenda lile alilolikusudia Mungu, mvua ikinyesha matokeo yake ni mimea kustawi, pale kuliko na nyasi kavu kunabadilika rangi ya kijani kibichi inaanza kuonekana kwasababu mvua ina neema na Baraka ndani yake, mvua ni Baraka kutoka kwa Mungu. Sasa anasema ndivyo itakavyokuwa Neno langu litokalo kwenye kinywa change.
 
Mungu anapotaka ulisikie Neno lake linaweza kuja kwa namna tofauti taofauti, wewe kinachokupasa ni kuwa makini na kusikiliza Mungu anachosema kwasababu linakuwa na kusudi lake kwako. Neno lake linakuja kwako ili liyatimize mapenzi yake Mungu, hakuna Neno linalokuja kwa kutimiza mapenzi ya muovu shetani  bali ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu tu, likija kwako linakuja kwa ajili ya mapenzi ya Baba aliye Munguni ili mapenzi ya Mungu yaweze kutumilika ndani mwako. Linaweza kuja Neno kwa ajili ya kukuonya, kukusaidia, au kukuelekeza yaliyo mbele yako, wewe unatakiwa uwe makini katika kilisikiliza Neno.
 
Sasa Neno la leo limekuja kukwambia Simama Katika Kweli ya Neno La Mungu. Simama katika kweli ya Neno la Mungu, ukiwa nje ya Kweli ya Neno la Mungu hutapata muongozo, muongozo wa kweli katika maisha yako unaupata unaposimama katika kweli ya Neno la Mungu. Unaposimama katika Kweli ya Neno la Mungu hapo ndipo unapojua ni nini Mungu anakuelekeza, Mungu akisema nataka kitu hichi kitendeke kwako au nataka unitumikie lazima uwe makini katika kutumika kwasababu Mungu ameleta Neno lake ili utumike. Faida ya mtu aliyesimama katika Neno la Mungu huwa ni kubwa sana kwasababu Neno la Mungu lina mamlaka kamili ndani yake, linamaliza mashauri ya wanadamu, ni Neno la Mungu tu ndilo linalo maliza dhiki,huzuni na kero  ya wanadamu, Ni Neno la Mungu tu ndilo linalokuja na mamlaka kamili.
 
Watu wanapata shida ni kwasababu hawasimami kwenye Neno la Mungu, uanpata shida kwasababu ndani mwako umejaza sana mambo ya hapa duniani zaidi ya Neno la Mungu. Neno la Mungu ni Ulinzi na ni Moto ulao.

No comments:

Post a Comment