''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, May 10, 2015

HATA KAMA UNAPITA KATIKA MAJARIBU MAZITO, USIMUACHE YESU


Mhubiri: Mwinjilisti Masokola
Neno: Ufunuo 1:9-11,2:4-7

Yawezekana umesikia majina mengi sana lakini hayawezi kuponya lakini Jina la Yesu Krist wa Nazareti aliye Hai linaweza kuponya. Usikimbilie kanisa bali mkimbilie Yesu tatizo lako unakimbilia kanisa lenye watu wengi, jibu liko moja tu kimbilia kwa Yesu tu hata kama utapitia katika majaribu au mapito magumu wewe mkimbilie Yesu tu.
 
Usijivunie mchungaji wako wala mtumishi wako, usijivunie dini yako bali jivunie Yesu Kristo aliyekuokoa. Usimuache Mungu hata kidogo maana hujui lini Yesu atarudi na  hii dunia itakunjwa kama karatasi lakini Jina la Yesu. Kanisa la leo umeacha upendo wa mwanzo, angalia wapi umeanguka. Wengine watabaki kwa ajili ya kuwawazia watu vibaya, wengine watabaki wakisengenya watu, Jina la Yesu kuna watu wanalichukulia kimchezo mchezo lakini Jina la Yesu ni ngome imara wenye haki hulikimbilia wakawa imara, hata kama unapita katika mateso lakini usimuache Yesu. Yohana alipita kwenye wakati mgumu mpaka akatupwa katika kisiwa cha patmo  lakini hakumuacha Yesu.

No comments:

Post a Comment