''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, May 24, 2015

KUKUSANYA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU

Mhubiri: Mchungaji Amos Kutoka Mwanza
Maandiko: 1Wafalme 20:21-22, Matendo 1:8, 2:4

Kwa kawaida Mtu mwenye nguvu siku zote anaheshimika, anaongoza na anatawala, pia mtu mwenye nguvu anajiamini, mwenye nguvu haogopi kitu. Ukijawa na Nguvu za Roho Mtakatifu kuna vitu utaamuru viondoke na vitaondoka, kuna vitu utaviambia vikuache na vitakuacha.
 
Tumesoma habari za mfalme wa Israel alivyotaka kujisahau baada ya kuwapiga washamu lakini nabii akamuonya. Ukishinda majaribu usijisahau sana kwasababu bado upo katika dunia hii na katika mwili huu bado vita viko mbele, mfalme wa Israel baada ya kushinda alikuwa kama anataka kujisahau kupumzika, bali wewe endelea kusoma Neno la Mungu zaidi, endelea kuhudhuria semina, na endelea kuomba kwa bidii, chukua tahadhari vita haijaisha, ukijisahau baada ya vita adui yako ataendelea kufanya mazoezi alafu baadaye gafla atakushinda lakini ukiendelea kukusanya nguvu za kutosha adui akija akukute bado uko vizuri. Jitaidi ule moto ile nguvu ya Roho Mtakatifu isizimike ndani yako. shetani atazidi kukutafuta lakini kama umezungukwa na Nguvu ya Roho Mtakatifu  hatakupata. Shetani akikutafuta asubuhi ,mchana, hata usiku hatakupata kamwe. Matendo 1:6-8 Yesu alijua bila hiyo nguvu hutaweza kuwa salama, kazini kwako, masomoni mwako hata kwenye maisha yako bila hiyo Nguvu bila hiyo nguvu utafeli.
 
Akawaambia mtapokea Nguvu 1Yohana 1:1-3, Matendo 2:1- kama unataka Nguvu ukaliwe na moto wa Roho Mtakatifu kila wakati, kanisa la kipentekoste na watu waliokoka ni kutunza nguvu ya Roho Mtakatifu. Ukiwa na Nguvu za Mungu kwa kadri utakavyoteswa au kukutana na misukosuko kama una nguvu za Mungu bado utasimama na kumbuka una vita kazini, shuleni, kwenye uchumba wako,kwenye ndoa yako Kutoka 1:8-12.

---------------------------------------------------------------------------------------
KONGAMANO LA PENTEKOSTE LAENDELEA, WATU WABUBUJIKA ROHO MTAKATIFU 

No comments:

Post a Comment