''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, May 3, 2015

SIKUKUU YA CHRISTIAN MEN'S FELLOWSHIP (CMF)

UJUMBE: KAA TAYARI KAMA BIBI HARUSI
Maandiko: Yeremia 2:32, Mathayo 25:1-13
Mhubiri: Ndugu Samweli Zayumba

Je bibi harusi anaweza kusahau harusi yake? hasha hawezi, na sisi kama bibi harusi  tusimsahau Mungu wetu, wana wa israel walimsahau Mungu wao na hapa Yeremia alikuwa anawakumbusha wana wa israel. Tambua umechaguliwa na Mungu, wokovu ni neema na ni wa bure, hivyo basi kama bibi harusi asivyoweza kusahau vazi lake na wewe usiweze kumsahau Yesu aliyekuokoa.
 
Mungu anachotaka ni kutuona na vazi la wokovu katikati ya watu wengine. Kumbuka kwamba upo safarini hivyo basi jiulize sasa Je wewe ni vuguvugu au moto? na unachukua hatua gani za kubaki kuwa moto yaani kuwa na Yesu?.
 
Mathayo 25:1-13, wapumbavu walikuwa na taa tuu lakini werevu walikuwa na taa na vifaa vya kuweka akiba ya mafuta lakini kumbuka wote walikuwa sehemu moja lakini badae wapumbavu wakafungiwa mlango nje.  
 
Hakikisha taa yako ina mafuta, na Taa ni Neno la Mungu na mafuta ni Roho mtakatifu. Yesu Kristo ndio Neno na Neno ndio taa yako (zaburi 119:105) ikimulika njia yako nguvu za giza hazitakaa mbele yako. Hebu jiulize kwanini unaweka mafuta kwenye gari?, ni kwasababu una safari ambayo iko mbele yako hivyo hivyo kwenye maisha ya kiroho uko safarini unahitaji Neno la Mungu ili uweze kufika unakotakiwa kufika. Kwanini unaishi kihasara tambua wewe ni bibi harusi kwahiyo tunza maisha yako usimuache Mungu hata kidogo. Mathayo 7:24 jenga juu ya mwamba ishi ukiwa juu ya mwamba na mwamba ndio Yesu Kristo. Tembea katika Neno la Mungu, ukitembea katika Neno la Mungu hutapotea katika masiha yako ya kiroho na ya kimwili pia. Ndugu kaza mwendo bado hujafika weka mafuta zaidi ambayo ni Neno la Mungu na kuwa na Yesu ambaye ni Mwanga wako, Biblia inasema tusipohukumiwa ndani mwetu tunaujasiri..

No comments:

Post a Comment