''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, April 26, 2015

NENO LA MUNGU

Mhubiri: Mr. Mwalongo
Maandiko: Mwanzo 1:1-5 

Neno la Mungu lina nguvu and uweza, na Yesu ndiye Neno la Mungu, Yesu ni Neno. Kama umejaa Neno la Mungu inamaanisha uko na Yesu na Yesu amejaa ndani mwako, lakini kama uko mbali na Neno la Mungu yaani neno la Mungu halijajaa ndani mwako inamaanisha kwamba uko mbali na Yesu na Yesu hajajaa ndani yako. 

Neno la Mungu lazima liwepo na lijae kwa wingi ndani yako lakini haliwezi kuwa kwa wingi ndani yako kama hautumii muda wako kulisoma neno la Mungu. Je ni kiasi gani cha muda wako unatumia kusoma neno la Mungu? ni kiasi gani cha muda wako unatumia kutafakari neno la Mungu?, lazima utumie muda kusoma neno la Mungu vizuri na kulielewa vizuri.

Kama neno la Mungu halijajaa ndani yako basi lazima kutakuwa na kitu kingine kilichoujaza moyo wako. Utandawazi usichukue nafasi ya Mungu nafasi ya kusoma neno la Mungu, yawezekana unatumia muda wako mwingi sana 'kuchat' au kuongea na simu, kuangalia mitandao mbali mbali, kuangalia luninga kuliko kusoma neno la Mungu, rekebisha ratiba yako, weka wa kutosha kwa ajili ya Neno la Mungu kilitafakari na kuomba. 

Mungu anaangalia ndani mwako haoni Neno la Mungu, haoni Neno lake ndani yako na anaumia anavyoona huna Neno lake ndani mwako maana anajua bila Neno la Mungu ambaye ni Yesu mwenyewe huwezi fanya lolote. 

Kila kitu kitapita lakini Neno la Mungu haliatapita, bila Neno la Mungu utapotea. Biblia inasema Neno la Mungu lijae kwa wingi ndani mwetu. Mungu hafurahii sisi kutokuwa na Neno la Mungu ndani mwetu, tuwe na Neno la Mungu ili hata tukijaribiwa tuweze kusema kama Yesu wakati ule alivyojaribiwa kwamba imeandikwa...(Neno fulani), lakini hutaweza kufanya hivyo na kumshinda shetani kama hujajaza Neno la Mungu kwa wingi ndani mwako. Ili uwe na ujasiri wa kusema kwamba imeandikwa...! ni lazima ujae Neno la Mungu. Neno la Mungu ni kila kitu linaponya, ni msaada wetu ukipitia kwenye kila hali unaweza kusema imeandikwaa...!! tujae Neno la Mungu.

1 comment:

  1. Nino la Mungu ni taa ya miguu yetu na mwangaza wa njia zetu, inamaana bila neno tunakuwa tunatembea gizani hivyo sio kwamba hatuoni tunapokwenda lakini tunapotea njia. watu hawajui hili lan neon la `mango lina uwezo pia wa kutakasa kwasababu ktk Yohana 17:17 Yesu mwenyewe anasema uwatakase na ile kweli, neno lake nadi kweli, na ujue yeye mwenyewe ndiye neno la Mungu (ufunuo 19:13)

    Bila nano huna nguvu ya kufanya jambo lolote ndio maana hata Yoshua baad ya kukabidhiwa majukumu ya Musa anaambiwa neno lisitoke kinywani mwake, `yeremia pia anawekewa neno mdomoni ili aweze kupanga na kung'oa. kutafakari neon la Mungu wakati wrote maana yake ni kumtafakari Mungu wakati wote. Huwezi kuomba bila kuwa na nano la Mungu. Tukisema tunayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu tunamaanisha kuwa tunayaweza yote kupitia neno la Mungu. Mungu anaweza kila kitu na yupo tayari kufanya kila kitu lkn lazima kiwe katika maenzi yake. Mapenzi ya Mungu ndio neno la Mungu. Mkristo hana nguvu nje ya neno la Mungu. Kumbuka imani inakuja kwa kusikia neno la Kristo na mambi yanataka imani so neno linajenga imani ya kuomba lkn pia linatuonyesha mipaka ya kuomba na namna ya kuomba na kupokea pia.

    ReplyDelete