''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, April 19, 2015

ENDELEA KUAMINI UTAUONA UTUKUFU WA MUNGU

Mhubiri: Mrs. Lucy Masembo
Maandiko: Yohana 11:1-6,17-40, Zaburi 78:40-48

Biblia inasimulia habari za hawa watu wa watatu Martha, Mariam na Lazaro jinsi walivyompenda Yesu. Hapa tunaona lazaro alikuwa hawezi na wakatuma ujumbe kwa Yesu kwamba rafiki yako umpendaye hawezi/anaumwa, lakini Yesu akaendelea kukaa kule alikokuwa na Yesu akawaambia kabisa wanafunzi wake kwamba lazaro ndugu yetu anaumwa na baadaye Yesu alipata ujumbe kwamba Lazaro ameshakufa lakini Yesu akawaambia hivi wanafunzi wake ndugu yetu amelala akimaanisha kuwa amekufa. 

Lakini kwanini Yesu akawie/achelewe?, yamkini hata wewe unamuomba Mungu kitu flani kwa muda mrefu mpaka imefikia mahali unajiuliza kwanini Yesu hakujibu? au kwanini anachelewa? lakini nakwambia Yesu hatakaa achelewe, Yesu yuko pamoja na sisi milele, ni kweli unaona Yesu anakawia lakini nataka nikwambie hivi Yesu anajua wakati sahihi wa kuleta jawabu la hitaji lako ambalo unamuomba, ukiendelea kungoja utauona utukufu wa Mungu. Yesu alijua wakati wa kuwajibu Martha na Mariam.

Ilikuwa ni lazima Lazaro afe ili watu wajue kwamba kuna uweza katika Kristo Yesu. Martha anamwambia Yesu umechelewa lakini Yesu alimwambia amini ufufuo na uzima, martha alielewa ni ule ufufuo wa siku ya mwisho, ilikuwa ni vitu viwili tofauti Yesu anaongelea ufufuo wa pale pale lakini Martha anazani ufufuo wa siku za mwisho, hakutambua kwamba Yesu yupo pale anayeweza kila kitu, kama yupo hapo Yesu unaweza kufunguliwa, akiwepo Yesu maana yake kuna kila kitu. 

vitu vinavyoweza kukuzuia 
1.Kuangalia hali/mazingira uliyonayo kutoka 14.. mapito yapo tu na ni lazima upite ili Yesu aonekane na ukuzwe imani yako, yawezekana upo na Yesu lakini inawezekana unaona kufa kufa tu kama tomaso wakati uko na Yesu kumbuka kwamba uko na Yesu , 

2.Kulinganisha tatizo ulilonalo na Yesu, martha na mariam walilinganisha tatizo waliokuwa nalo na Yesu, waliona kifo ni kikubwa kuliko Yesu Hesabu 13:..

3.Kumpa Mungu mipaka, ya kwamba anaweza hapa tu na kitu fulani hawezi, martha alimpa Mungu mipaka martha alimwambia Yesu lazaro alishakuwa kaburini siku 4, hakutarajia kama Yesu anaweza fanya jambo kuhusiana na hilo. zaburi 78:40-48

 

No comments:

Post a Comment