''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, April 12, 2015

UMOJA KATIKA YESU



Maandiko: Yohana 17:20-23, Zaburi 133:1-3
Mhubiri: Mzee kiongozi, Dr. Mumghamba

Umoja kati yetu, umoja kati ya familia na umoja kati ya kanisa, huwezi kuwa na umoja na mwenzako kama hujamsamehe au kama una kinyongo nae, na kama una kinyongo na mwenzako hutaweza kumshirikisha jambo lako mwenzako.  Yesu aliongelea umoja kama kitu muhimu sana katika maisha yetu na zaidi sana kwa sisi tunaomwamini. Yesu alituombea kwa Mungu tuwe na umoja ndani yake kama Yeye na Baba yake walivyokuwa wamoja. Umoja katika Yesu na sio umoja pamoja na Yesu, alitaka wewe uwe ndani Yake na Yeye ndani yako ili wote tuwe na umoja katika Yeye (Yesu) na tukishakuwa wote wamoja katika Yesu ulimwengu utaona kazi kubwa aliyokuja kuifanya na ya kwamba Mungu alitupenda sisi sana kama alivyompenda Yesu mwanae. 

Kanisani mnaonana na kukaa wote pamoja lakini yawezekana hamna umoja kati yenu wote, mume na mke wanaweza wakaishi pamoja lakini yawezekana hawana umoja kati yao, familia yaweza kuishi pamoja lakini wasiwe na umoja kati yao. Kwahiyo kukaa pamoja au kuishi pamoja sio mara zote ikamaanisha umoja kati yenu.

Yesu alivyoongelea umoja hakumaanisha umoja huu wa kawaida lakini umoja wa kiroho ambao ndani ya umoja huo tunapata kubarikiwa na pia kuwa na uzima tele (zaburi 133:3).
Ukimruhusu Yesu kukaa ndani yako na wewe ukikaa ndani yake kisawasawa hutapata shida wala hutasukumwa na mtu kumpenda mwenzako, kama kila mtu katika familia au kanisa akikaa ndani ya Yesu na Yesu ndani yao moja kwa moja familia au kanisa litakuwa na umoja.

No comments:

Post a Comment