''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Friday, April 3, 2015

YESU ALITOA MAISHA YAKE MWENYEWE KWA AJILI YAKO

Mhubiri: Mch. Mainoya
Maandiko: Mathayo 26:36-50,27:11-31, Luka 23:33-47

Hapa tunaona Yesu Kristo ameenda Gethsemane, alienda kwa kule kwa ajili ya kuomba baada ya kumaliza kushiriki chakula cha mwisho na wanafunzi wake na alipomaliza alishajua sasa saa. Bwana Yesu alikuwa ni mwana maombi na alimtegemea Baba yake wa Mbinguni katika yote, Bwana Yesu alikuwa kwa ajili ya kutenda mapenzi ya Mungu basi, na alijua anakwenda kukinywea kikombe cha mateso ambacho hatakiweza ila kwa msaada wa Mungu, alimtegemea Mungu katika mateso yale, ikiwa Yesu mwana wa Mungu alimtegemea Mungu katika mateso yale Je si zaidi sana sisi tumtegemee Mungu katika mateso yetu na shida zetu!

Tunaona Yesu aliwaeleza yale yaliyo mbele yake wanafunzi wake watatu ili waombe pamoja nae, alitaka waombe pamoja nae usiku ule, mtu ukiwa pekee yako nguvu inakuwa ni kidogo unamwambia ndugu yako niombee jamani naumwa ili atakavyoomba nguvu itakuwa nyingi na Yesu alitegemea hivyo hivyo alijua wale wanafunzi watatu aliotembea nao sehemu nyingi watasimama pamoja naye katika maombi lakini cha ajabu ni kwamba wale nao walishindwa wakalala.
 
Tunapoomba lazima tuweke nafasi ya mapenzi ya Mungu, Mtegemee Mungu tu katika shida yako, tukeshe kuomba ili tusiingie majaribuni, kuna mahali pia na sisi tunatakiwa kunyamaza kimya kama Roho Mtakatifu atakavyo kuongoza, wokovu haukupatikana kirahisi tu usichezee wokovu wako, Yesu alitoa maisha yake mwenyewe kwa ajili yako.

No comments:

Post a Comment