''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, March 29, 2015

MUNGU ANAYO NAFASI YAKO KATIKA MPANGO WAKE WA UKOMBOZI

Mhubiri: Mrs. Emmaculate Nigula (Global Harvest Theological Seminary) 
Maandiko: Mwanzo 12:1-3, Mwanzo 3:15


Mungu anayo nafasi au sehemu yako katika mpango wake wa ukumbozi, nilipokuwa naandaa somo hili nikakumbuka hadithi ya binti mmoja ambaye miaka 22 iliyopita akiwa anasoma kidato cha tano alimpata Yesu/aliokoka akiwa shuleni, wakati huo huyu binti alikuwa ana miaka 21, alivyookoka familia yake haikukubaliana na hilo jambo, kwahiyo familia ile ikamtenga, ikamtenda na kumsukasuka mpaka ikafikia mahali baba yake akamshikia panga kwa kisa cha kufukuzwa shule kwasababu amekoka, lakini baada ya kipindi fulani Mungu alimsaidia akarudi shuleni kwenda kusoma Diploma yake ya ualimu kwa miaka miwili na baada ya kufanya kazi kwa mwaka mmojaakawa amepata wito na kuitika wito alioitwa na Mungu akaamua kwenda kusoma chuo cha Biblia kwa miaka 4, yule binti alipotoka chuoni akaenda kwenye utumishi na Mungu akampa neema ya kuwafundisha na kuwaanda watumishi Mungu kitu ambacho hakukifahamu kabisa wakati ule akiwa anampokea Yesu na kupitia katika misukosuko, hakujua kabisa kwamba Mungu ana muandaa ili kuwafundisha watumishi wake na pia kuwa baraka katika ile familia iliyomtenga na kwa ndugu zake na kwa watu wote, maana ile familia iliyomtenga na kumfukuza nyumbani na kaka na dada zake waliomtukana matusi hivi leo wote wameokoka. Na huyo binti ndio huyu anayekuletea hili Neno la leo (Mrs. Emmaculate).

Unapo amua kumkubali Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako yaani kuokoka huwezi jua ile NDIO uliyoisema kwa Yesu na kukubali kuokoka itakuchukua kiasi gani au itakufanya uwe nani huko mbele na itakupitisha katika mapito gani. Yule binti hakujua ile ndio yake aliyokubali kuokoka itamfanya apitie katika jaribu la kutengwa na familia yake Lakini baadae kuwa baraka sana sana kwa familia yake na sio familia yake tu bali na watumishi wa Mungu na watu wote. Ndio maana ujumbe wa leo unakwambia kwamba Mungu anayo nafasi yako wewe hapo katika mpango wake wa ukombozi, yule binti hakujua kwa wakati ule kwamba Mungu anamuokoa ili kupitia yeye aokoe familia yake nzima iliyokuwa inashiriki ibada za kimila.

 Mungu anayo nafasi yako katika mango wake wa ukombozi, na mpango huu Mungu alikuwa nao tangia zamani haukuja tu hivi hivi, alijua huko mbeleni binadamu atakuja kumuacha kwahiyo akaandaa mpango huo na katika Mwanzo 12:1-3 tunaona Mungu alianza mpango wake kwa kumtenga Abrahamu kutoka kwenye familia yake.
 
1. Mungu alimtenga, amekutenga ili aweze kutembea na wewe 
2. Mungu amekubariki ili uweze kuwa baraka kwa wengine sio baraka ya majumba au magari bali baraka ya wokovu 
3. Mungu amekuteuwa ili kuwa mkondo wa baraka za ibrahim ambao ni wokovu.

No comments:

Post a Comment