''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, August 30, 2015

YESU ALIFANYA VITU AMBAVYO WENGINE HAWAKUWEZA KUFANYA

Mhubiri: Mch. Mitimingi
Maandiko: Mathayo 14:25-33

1.Yesu alitembea juu ya maji lakini wengine walitembea kwenye boti, Mathayo 14:25-33 Yesu alitembea juu ya maji na sio kwenye barabara tofauti na wanadamu wengine, tumeshazoea watu wanasafiri juu ya bahari kwa meli lakini Yesu alitembea juu ya bahari, na sisi alitupa hiyo nafasi kwasababu ndani yetu tunaye Yesu tunaweza kutembea sehemu ambazo wengine hawawezi tunaweza kufika mahali ambapo watu hawafiki tunaweza kufika, tunaweza kufanya mambo ambayo wengine hawawezi kufanya kwasababu tunaye Yesu.
 
Wanafunzi wa Yesu walimuacha Yesu wakatangulia wenyewe na mashua, walipomuona Yesu anakuja huku akitembea juu ya maji wakaogopa na kupata hofu kwasababu walizani ni kivuli/mzuka, hata wanafunzi wake Yesu ambao walikaa na Yesu muda mwingi lakini hawakuamini kuwa yule aliyekuwa anatembea kwenye maji kuwa ni Yesu hicho kitu ndicho kinachotokea hata leo, ni kweli unajua kuhusu Yesu, unajua Yesu kuwa ana nguvu sana na ana uwezo wa kufanya kila kitu lakini unapokuja ugonjwa wa aina fulani unasema huu ugonjwa hauwezi kupona kupitia Yesu ni mpaka kitu fulani, unaanza kusema hii saratani haiwezi kupona kwa kuombewa ni mpaka kitu fulani, unamuwekea Yesu mipaka unamuweka Yesu ndani ya boksi kwamba aina fulani ya ugonjwa Yesu anaweza kuponya lakini aina fulani hawezi au haiwezekani. Mfano mtu akishuhudia alikuwa anaumwa kichwa akamuomba Mungu akamponya watu watashangilia, lakini akija mtu akashuhudia nlikuwa kiwete nilikuwa sina mguu lakini namshukuru Mungu baada ya kumuomba akaniponya sasa nina miguu yote miwili badala ya watu kushangilia wataanza kunong'onizana mh! huyu atakuwa muongo hakuwa kiwete.
 
 
Petro aliweza kutembea juu ya maji kwasababu alikaza macho alimtazama Yesu tu lakini alipobadili muelekeo wake kuangalia upepo hapo ndipo alipoanza kuzama. Ukikaa na Mungu kwa uaminifu Mungu atakuwezesha kufanya mambo makubwa zaidi ya vile ulivyofikiri na zaidi ya uwezo wako lakini Mungu hakuwezeshi kufanya hayo ni kwasababu umeacha kumtazama Yeye umeacha kusikiliza sauti yake, umeacha kumsikiliza Roho Mtakatifu na kuamua kuangalia upepo kuamua kuangalia matatizo uliyonayo, na ukishaanza kuangalia upepo/shida iliyonayo hapo ndipo woga utaanza kukuingia na ndipo utaanza kuzama ndipo utaanza kurudi nyuma kiroho. 

No comments:

Post a Comment