''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, September 21, 2015

UNYENYEKEVU WA WANA WA MUNGU

Mhubiri: Ndg. Frank Mwalongo
Maandiko: Wafilipi 2:1-11, Mathayo 18:1-4

Neno unyenyekevu linamaanisha nidhamu ya hali ya juu, utulivu wa hali ya juu wa kimungu. Tunajifunza unyenyekevu kutoka kwa Kristo mwenyewe maana Yeye ndiye mfano wetu. Yesu alikuja kutoka mbinguni alishuka na kujinyenyekeza akaacha utukufu mkuu sana akaja ulimwenguni.
Hakuna unyenyekevu zaidi ya alioufanya Kristo Yesu lakini hakuishia hapo tu, bali alichukua maovu yetu dhambi zetu na akamwaga damu yake kwa ajili yetu. Alimtii Baba akakubali kuvaa mwili wa mwanadamu akatemewa mate akaaitwa mnyang'anyi, akafa na kufufuka kwa ajili yetu, kwahiyo Mungu Baba alifurahia unyenyekevu ule mkuu na akaamua kulituuza sana jina la Yesu kuliko majina yote mbinguni na dunia, jina lipitalo majina yote. 
Na wewe kama mtu wa Mungu inakupasa uwe mnyenyekevu kwasababu usipokuwa na unyenyekevu ukaidi au kiburi kitakuwa ndani yako ndio maana huwezi kunyenyekea huwezi kumtanguliza mwenzako kabla yako. Na unyenyekevu huu hautakiwi uwe unyenyekevu wa nusu nusu,bali unyenyekee na kuhesabu mwenzako kuwa ni bora kuliko wewe mwenyewe.
Ukinyenyekea utakuwa unakuja ibada za katikati, ukiwa mnyenyekevu utafuata na kutimiza ratiba zote za kanisani. hebu jiulize je unamnyenyekea Kristo? watakatifu tupige hatua, ukitaka kwenda mbinguni jinyenyekeze mbele za Mungu na ukifanya hivyo ule uana wa Mungu unakamilika kweli na baaada ya kufanya hivyo ahadi zote Mungu alizoahidi zitatokea kwako, na sio unyenyekevu nusu nusu bali unyenyekevu wa kijumla. Hebu jitathimini Je umemtii Bwana kiasi gani?,  ile nafasi ya utii unyenyekevu ukaidi utaingia au kiburi kitaingia, ukiambia kuna maombi ya kufunga funga kwa bidii, ukiambiwa kufunga siku 7 funga siku zote saba na sio nusu yake 

No comments:

Post a Comment