''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, October 12, 2015

SIRI YA KUKAA MIGUUNI PA YESU

Mhubiri: Mch. Mhini
Maandiko: Luka 10:38-42
Moja ya mambo muhimu katika maisha ya mwamini ni kugundua siri ya kukaa miguuni pa Yesu. Siri hiyo alipewa neema ya kuijua Mariamu umbu lake Martha. Kijiji cha Bethania yalikuwa ni maskani ya ndugu wa pamoja ambao walikuwa maskini. Bwana Yesu aliwapenda ndugu hawa na mara kwa mara aliwatembelea, na hapa ndip maskini Lazaro aliyekuwa ndugu wa hawa dada wawili alikuwa hawezi.
 
Hangaiko la utumishi mwingi lilikuwa ndani ya Martha aliyenung'unikia hatua ya mariamu kusikiliza mafunisho ya Yesu Kristo. Suala la kusikiliza maneno ya Yesu Kristo limekuwa adimu kwa baadhi ya watakatifu. Muda wa kujitoa kwa ajili ya mafundisho ya Neno la Mungu kwa walio wengi ni adimu. Shughuri za mara kwa mara za kutafuta maisha zimechukua nafasi kuliko kukaa miguuni pa Yesu.
 
 

No comments:

Post a Comment