''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, December 28, 2015

MWENYE HAKI HUOKOLEWA KATIKA DHIKI

Mhubiri: PASTOR CHARLES WANDWI.
Maandiko: Zaburi 34:19,Isaya 45:22

Mungu wetu ni Mungu ambaye yupo wakati wote na anafanya kazi wakati wote. Mimi na wewe Mungu hutukuokoa kutoka kwenye mateso mbalimbali kwa kuweka mbadala wake katika mateso hayo.
Mambo yote kwa Mungu yanawezekana pale utakapoamini tu. Ukiamini utapokea uponyaji na kila utakachomuomba Yeye lakini usipo amini hutapokea kitu.

Tenda haki ya Mungu upokee muujiza wako, kuwa mwenye haki mkamilifu na Mungu atakusaidia katika shida yako na atakujibu mahitaji yako, mara nyingine yawezekana umemuomba Mungu sana kuhusu jambo fulani huoni jibu lakini hebu jaribu kujiuliza je wewe unatenda haki mbele za Mungu?, je unaishi maisha matakatifu?, dhambi huzuia maombi yako kujibiwa, acha kuishi maisha ya uvuguvugu amua leo kuwa moto na Mungu atakuonekania .

Mungu anajua dhiki,mateso na kila aina ya shida unazopitia katika maisha yako,anachohitaji ni wewe tu umkaribia Yeye. Unapobaki unalia Mungu amekuacha, je haki ya Mungu umempa?.
 
Mungu anaposema mtakatifu anamaanisha ni mtu aliyetengwa mbali na dhambi. Kama umemuacha Mungu usitegemee kuwa utapata majibu ya Mungu kwa mahitaji yako.
 
"Ministry hailei, ni kukuondolea kile ulichonacho bali kanisa ndipo palipo na malezi."
Watu wengi wanatafuta njia ya mkato,lakini  Kwa Mungu hakuna njia ya mkato na Mambo yake yamenyooka."

Mungu anachotaka kuona katika kanisa lake ni kuishi maisha Matakatifu. Ukiwa ni mwenye haki na unaishi maisha yaliyo matakatifu Mungu hatokuacha uangamie. Yupo Yesu mnazalethi aliye hai ambaye anaponya na anagusa na kufungua watu wake. Mkubali Mungu na ukae nae sawasawa naye hatakuacha. Hakuna jambo linaloshindikana kwa Mungu aliye hai.
Mungu wetu si mganga wa kienyeji,Ni MUNGU wa utaratibu.

Katika zaburi biblia inasema mwenye haki hautoachwa kamwe bali utakumbukwa milele. Dhambi inauma kama meno, inaua, dhambi ni mbaya. Mungu anahitaji utakatifu kwa watu wake. Ili  bwana aweze kukuokoa kwanza ni kutengeneza maisha yako yawe sawasawa na mapenzi ya Mungu. Z
aburi 34:19, Tembea katika neno la Mungu nawe utamwona Mungu na ukiacha neno la Mungu utamuona shetani. Uwe na cheo cha aina chochote ama huna cheo neno ni moja tu,ACHA DHAMBI. Maisha ya mwenye haki yanamuhitaji sana Mungu ili kuwa na uvumilivu na mwisho kuona yale Mungu aliyotuandalia, Isaya 45:22
 
MAMBO YAKUFANYA KUISHI MAISHA MATAKATIFU
1.Usitende dhambi
2.Uishi maisha Matakatifu
3.Mpende Bwana wako kwa nguvu zako zote na akili zako zote
4.Mpende jirani yako kama nafsi yako
5.Kuwa na Roho ya Msamaha
6.Maisha yako yatawaliwe na Roho Mtakatifu
7.Kuwa na Bidii ya Maombi
8.Kubali Kumtumikia Mungu katika Huduma AliyokupaNo comments:

Post a Comment