''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, February 28, 2016

MTAKATIFU AZIDI KUTAKASWA

Mhubiri: Mch.Rozina Janga
Maandiko:Ufunuo 22:8-12


KWA NINI MTAKATIFU NA AZIDI KUJITAKASA?
Ni kwa sababu tuko katika ulimwengu huu bado mavumbi ni mengi yanayotufumba juu ya utakatifu wa Mungu.


JE TUNAJITAKASAJE?
Je, ni kwa kwenda kanisani?
Kanisa ni mimi na wewe kwahiyo ni mimi na wewe hapo tunaotakiwa kutakasika/kujitakasa wakati wote.

ROHO MTAKATIFU habadiliki. Unapokuwa mchafu(unatenda dhambi) ROHO MTAKATIFU anaugua na MUNGU  mwenyewe anaugua. Jitahidi kwa jitihada zozozte zile kuwa mtakatifu mbele za Mungu na mbele za watu pia.
 
Wewe kama mtu uliyeokoka ni barua mbele za watu, Jiulize je jinsi unavyovaa unaonekana kama umeokoka? maneno unayoongea na matendo unayofanya kunamuwakilisha Yesu?. Acha kabisa kuipaka rangi dhambi yaani kutenda dhambi na kuitetea tetea, dhambi ni dhambi tu hakuna dhambi ndogo wala kubwa, ndugu yangu usikubali kutenda dhambi bali kuwa mtakatifu na uzidi kujitakasa. Tujiangalie kwamba maisha yetu yanaendaje?,mwenendo wetu unaendaje?. MUNGU anataka atuone sisi ni watakatifu siku zote na ni lazima tusimame MUNGU atuone kwa utakatifu wetu.

Unapoingia kanisani malangoni mwa mahali pa kumuabudu MUNGU wetu hebu jiangalie mwenendo wako na maisha yako.
Warumi 6:19

Kanisa na tuwe waangalifu na mambo ya sasa tusije tukatoa kanika utakatifu wa MUNGU na kuingiza mambo ya dunia. Kabla hujaondoka nyumbani kwenda mahali popote na hata huko ulipo jiulize je wewe ni mtakatifu. Msikilize ROHO MTAKATIFU anachokwambia unapohitaji kufanya kitu chochote ili uzidi kutakasika na kuwa mtakatifu.

"KILA MTU ATALIPWA SAWASAWA NA KAZI YAKE ILIVYO",hakuna atakayelipwa sawasawa na kazi ya mume/mke/ mzazi wako au mtu mwingine. Watakatifu waliopo duniani Mungu ndio anapendezwa nao na anasema hao ndio walio bora. Pia kwenda mbinguni ni lazima utafute AMANI na watu wote. Lakini pamoja na kuwa tunatakiwa kuwa na amani pia Mungu anakaa mahali patakatifu.

No comments:

Post a Comment