''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, June 27, 2016

KUISHI KWA IMANI

Mhubiri: Mr. Kinabo
Maandiko: Habakuki 1:1-4
 
Wakati huu Habakuki alikua na maumivu ndani yake kutokana na mwenendo wa maisha yake hata kumuuliza Mungu kwa habari ya maisha yake. Hata kwako pia jambo hili linawezatokea hata kufikia kuumia na kuwa na uchungu ndani yako juu ya maisha yako mwenyewe.

Mara nyingi unaona kuwa haki haitendeki na unamuomba Mungu na hakuna jambo linalotokea, kama mwanadamu unawezafikiri mengi lakini yatupasa kuishi kwa Imani.
Zipo hatua za kutuwezesha kuishi katika imani.
Tunapo omba kwa Mungu tunatakiwa kuamini kuwa hakika Mungu atafanya lakini wakati gani Mungu atafanya Yeye ndio anayejua majira na wakati.

Habakuki 2:2-4.
Ukifikiria kwa Abrahamu, Alisubiri miaka mingi hata kuona mambo ya Mungu na ahadi zake zikitimia. Tunatakiwa kuishi kwa imani tukiamini Mungu atafanya tunapoomba.
Habakuki  3:16-19.
 
Wakati Yesu yupo duniani na Lazaro amelala, dada wa lazaro walilalamika sana wakimlilia Yesu kwamba angewahi kufika basi Lazaro asingekufa. Ili kuishi katika Imani imetupasa kufanya mambo haya:

1.Kuendelea kuomba (Kumuomba Mungu wakati wote.)
Wakati tunaomba tunatakiwa kuwa makini maana Mungu anaweza akatumia njia tofauti na unayodhani wewe katika kukujibu ombi ulilomuomba. Pia tujue kuwa wakati wa Mungu kujibu ni wakati ulio sahihi unatakiwa kumuamini Yeye tu katika lile unalomuomba.
Efeso 4:17-24

Siku za Leo uelewe kwamba tunatakiwa kuishi kwa Imani mbele za Mungu.
1.Kuishi kwa Imani ina maana kusubiri Mungu atoe jibu.
2.kuishi kwa imani ina maana kumtii Mungu katika changamoto ya aina yoyote.
3.Kuishi kwa Imani ina maana kumwamini Mungu

No comments:

Post a Comment