''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Saturday, June 18, 2016

UTHAMANI WA KUWA MFUASI WA YESU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Mathayo 4:18-22

Huu ni wakati ambao Yesu alikuwa anachagua wanafunzi wake. Yesu aliwaambia njoo umifuate. Yesu alitaka awapate wafuasi wake au wanafunzi wake, tangu siku ya kwanza ulivyookoka ulikuwa mfuasi wa Yesu au mwanafunzi wa Yesu, na kwasababu umekuwa mfuasi wa Yesu ni wajibu wako kufuata vitu vyote na kufanya mapenzi yake yote.
 
Kwahiyo kama wewe ni mfuasi inamaanisha una kitu cha kufanya kwa ajili ya Bwana Wako na baadhi ya vitu hivyo ni:

1. Beba msalaba wako na umfuate Yesu Luka 14:27,
Kubeba msalaba inamaanisha nini?
Ni kukana maisha yako kwa ajili ya Yesu, kwa ajili ya kutangaza habari ya Yesu pia ni kuacha yale maisha yasiyompendeza Mungu kwa ajili ya Mungu. Mwanafunzi lazima uonekane kama unamfuata Yesu na mwanafunzi lazima ujazwe Roho Mtakatifu, na Kama huna Roho Mtakatifu jitahidi sana sana kumpata.

2. Lazima uwe unapenda Mungu na kupenda wenzako.

3. Lazima uwe mtii kwa chochote anachosema Bwana wako, kuwa tayari kutii chochote anachokuagiza Yesu hata kama hukipendi.

4. Lazima uamini mafundisho na kanuni za Yesu, Kama Yesu amesema usifanye dhambi basi usifanye dhambi, kama amesema shuhudia basi nenda kashuhudie.

5. Lazima uwe unajisalimisha kwa Yesu, ujitoe jumla kwa Yesu.

6. Lazima uwe na umoja wa Roho, sisi kama watu tulio okoka ni mwili mmoja kwahiyo ni lazima tuwe na umoja, kama hamna umoja hakutakuwa na kazi nzuri ya mwanafunzi.

7. Lazima ujitahidi kuishi kama Bwana wako Yesu alivyoishi, Yesu alikuwa muombaji mpaka maombi ya mkesha akiwa milimani, alikuwa na upendo, huruma, alisambaza injili, aliwapa msaada wahitaji.

8. Lazima uwe tayari kuilinda imani ya kiKristo, lazima uwe tayari kuitetea imani yako hata kama kwa kuwa tayari kufa kwa ajili ya Yesu Kristo.
 
Sisi kama Wanafunzi wake lazima tufanye kazi ya Yesu. Tambua kwamba kuna gharama ya kuwa mwanafunzi wa Yesu, kuwa tayari kwa lolote kwa ajili ya Yesu.

Je ni mara ngapi umeamua kwa kumaanisha kutoka moyoni kufanya kazi ya Mungu? Amua kubadilika sasa na ufanye kazi ya Mungu. 

No comments:

Post a Comment