''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, June 12, 2016

CHANGAMOTO ZA MAADILI YA WATOTO KUPOROMOKA.

Mhubiri: Mchungaji na Mwalimu Peter Mitimingi
 
1.Watoto kulelewa katika mwenendo wa kutofanya kazi za mikono.
Mtoto aliyelelewa kwa jinsi ya kutofanya kazi za mikono nyumbani hata atakapokuwa katika kazi atashindwa kufanya kazi na atakuwa mzigo.
Wafilipi 4:12
Watoto wanatakiwa waandaliwe katika hali zote. Mungu wetu ni Mungu wa mlinganyo tangu uumbaji wake. Hata katika maisha ya watoto wetu wanatakiwa kufundishwa maisha ya aina zote ya kufanikiwa na maisha ya kutofanikiwa, maisha ya kushiba na maisha ya kuona njaa, maisha ya kuwa na vingi na Maisha ya Kupungukiwa.

Watoto usiwadekeze kwenye maisha ya aina moja bali wajue maisha ya aina zote. Watoto hawataishi maisha yao shuleni tu, ipo siku wataishi maisha halisi hivyo ni vizuri kuwaandaa maisha ya aina zote, bila kubagua kazi watoto wa aina zote wanatakiwa kufanya kazi za aina zote.
 
2.Soko hulia na baadhi ya michakato ya mikataba ya kimataifa.
Kuna baadhi ya mikataba ya kimataifa inayoingilia malezi ya watoto. Mwanadamu ni lazima aishi kwa sheria na ajue akienda kinyume na sheria ajue ni nini matokeo yake. Watoto wanatakiwa wawe na nidhamu, na ili kupata nidhamu watoto hawa moja ya njia ya kumpa nidhamu ni kiboko. Mtoto anapolelewa katika maisha yasiyo ya nidhamu huharibika
 
Nguvu ya fimbo na nidhamu.

A. Wazazi wasipowarudi watoto wao wanawafanya watoto kuwa watoto wa wanaharamu(wasiostahimili). (Waebrania 12:7)
-kama kweli unampenda mtoto wako shika kiboko mahali anapofanya kosa na uwe wakati wa adhabu na sio kumchekea.
-Watoto wanatakiwa kujua kwamba hawapaswi kufanya vibaya na wakifanya vibaya kuna maumivu yatakuja mbeleni.
 
B. Mzazi aimyime mtoto mapigo kwani ni msaada wake wa sasa na wa baadae.(Mithali 23:13)
 
C. Maumivu ya fimbo ndiyo yanayosafisha uovu wa mtoto kutokea ndani kuja nje.(Mithali 20:30)
-Mtoto asiyechapwa atakuwa na maovu ndani yake.
-Wazazi wanapotoa adhabu wanatakiwa kwa pamoja wakubali adhabu iliyotolewa na sio mmoja anajenga na mwingine anabomoa.
 
D. Mtoto anayepewa nidhamu na mzazi anaokolewa na kuzimu(Mithali 23:14)

E. Kifaa kinachoondoa upumbavu kwa mtoto ni fimbo.(Mithali 26:3)
 
F. Fimbo inaleta hekima kwa mtoto.(Mithali 19:25)
-Huleta hekima na busara lakini mtoto asiyepata fimbo atawaaibisha wazazi wake, yeye mwenyewe, taifa lake na kanisa

MAMBO MATANO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUTUMIA FIMBO
1.Eneo la kumchapa mtoto wako.
2.Utatumia kifaa gani kumchapia mtoto wako.
-Usimpige mtoto wako kwa kibao.
-Usimpige mtoto kwa mateke
-Usimpige mtoto kichwa
-Usimpige motto kwa kutumia Magongo, wala Malungu, wala Kisu, Mti, Maji ya moto, Kumfunga kamba.
"ADHABU KAMA HIZO ZINAZIDI KUMBOMOA MTOTO NA SI KUMJENGA".
3.Wakati gani unamchapa.
-Usimchape mtoto wakati wa hasira(unapokuwa na hasira.)
-Usimchape mtoto mbele ya wageni au marafiki zake.*Atakapokutana na hao atajisikia mnyonge
-Usimchape mtoto mara kwa mara.
-Usimchape mtoto akiwa usingizini.

No comments:

Post a Comment