''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, July 31, 2016

JIFUNZE KUTAMBU NYAKATI NA MAJIRA

Mhubiri: Mch kiongozi Abdiel Meshack Mhini
Maandiko: Luka 12:35-40,54-57
 
Utayari ni kitu muhimu, maandiko yanasema jiwekeni tayari kwa kuwa saa msiodhani ndio anayokuja mwana wa Adamu. Bwana Yesu anarudi,lakini je umejifunga kiuno?, atakukuta uko tayari?. Mwana wa Adamu anauliza imekuwaje mtambue majira ya dunia hii na wala msitambue saa ya kuja mwana wa Adamu.

Bwana Yesu akatoa mfano mwingine katika kitabu cha Mathayo 25:1-13, huu ni mfano ambao Bwana Yesu aliutoa uliohusu watano wapumbavu na watano wenye busara, leo hii kuna kila dalili ya kurudi kwa Bwana Yesu lakini miongoni mwa watakatifu wapo watu wasiotambua hili.

Je, Bwana Yesu atakukuta upo tayari? Bwana Yesu amekuokoa lazima taa yako iwake, na ili taa iwake maana yake uwe na mafuta na mafuta ni Roho Mtakatifu, sasa kama huna mafuta maana yake hujajiandaa kumlaki Bwana Yesu, ambaye ndie aliyefananishwa na Bwana Harusi katika mfano ule wa watano wapumbavu na watato wenye busara.

Umekuwa unashiriki mahubiri na semina na makongamano lakini taa yako haina mafuta huna Roho Mtakatifu. Ni hasara iliyoje itakayokupata kwa kushindwa kujua nyakati na majira uliyonayo, na kwa sababu hiyo utashindwa kumlaki Bwana Harusi ambaye ni Yesu Kristo.

Unapozidi kukosea kila siku ni kwa sababu taa yako haina mafuta, mambo yako hayafanikiwi ni kwa sababu taa yako haina mafuta. Hii ni hasara mbele za Mungu. Amua leo kutubu ili Bwana Yesu atakapokuja akanyakue kanisa(wewe) likiwa safi na takatifu.

Jiandae taa yako iwe na mafuta maana habari ya saa ile hakuna ajuae hata malaika mbinguni.

Haya  ni mambo makubwa ambayo Bwana alikumbusha kanisa, wewe kama mwamini jiweke tayari kulakiwa na Bwana Yesu ili atakapokuja akukute ukiwa tayari.

Mambo yakupasayo kufanya ili taa yako iwake ni;-
1. Ishi Maisha Matakatifu.
2. Soma Kwa Bidii Neno La Mungu.
3. Uwe Mwaminifu Hata Katika Mambo Madogo.
4. Jifunze Kutambua Nyakati Na Majira Uliyonayo.

Wale watano wapumbavu waliiona hasara ya kutokuwa tayari na wale watano wenye busara waliiona faida ya kuwa tayari. Kwa nini uchanganyikiwe na vitu vya dunia vinavyopita?

Hivyo vitapita lakini Bwana Yesu hatapita. Jifunze Kutambua majira na wakati ulionao.
Kupitia maandiko haya ujue moyoni mwako sasa ni wakati wa kurudi kwa Mungu na kuwa tayari kumlaki Bwana Yesu. Jichunguze na utambue je wewe una mafuta ya taa yako kwa ajili ya kuwa tayari kumlaki Bwana Yesu? kwa nini ushindwe kuwa mkweli? kwa nini ugombane na watu wengine? unakumbushwa leo urudi kwa Bwana. Bwana Yesu anahitaji ujijazie mafuta wewe mwenyewe kwa kutambua makosa yako na kurudi.

Mafuta ni Roho Mtakatifu, yakupasa ajae ndani mwako tangu sasa na taa yako iwake ukawe tayari kumsubiri Bwana Harusi.

No comments:

Post a Comment