''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, August 14, 2016

MAISHA NDANI YA ROHO MTAKATIFU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini.
Maandiko:Matendo 1:4-5, Zaburi 1:2
 
Tunaposema kwa habari ya Roho tuna maana ya Roho Mtakatifu. Kila mwamini anapaswa kuishi  na Roho Mtakatifu. Yatupasa kujua umuhimu wa Roho Mtakatifu. Tunahubiri injili kwa sababu ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Wanafunzi wa Yesu waliambiwa wasitoke Yerusalemu kabla ya kupokea nguvu ya Roho Mtakatifu, kwa sababu wasingeweza kufanya kazi ya Mungu bila nguvu ya Roho Mtakatifu.

Kama huna Roho Mtakatifu shetani atakujaza mawazo yasiyo na utakatifu. Sababu kuu ya kanisa siku za leo kushuka kiutendaji ni upungufu wa Roho Mtakatifu ndani ya watu. Roho Mtakatifu ni wa milele na sio wa siku moja bali kila siku.

Ukikosa nguvu hii ya Roho Mtaktifu shetani atakuja na kukuondoa katika utakatifu, bali ukiwa na nguvu ya Roho Mtakatifu shetani hataweza kukusogelea kukuondoa katika utakatifu.
 
Mambo ya kuzingata kwa kanisa
1.Kuishi kwa kila neno litokalo kwa Mungu na nguvu ya Roho mtakatifu
Zaburi 1:2 "Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku".
2.Kutunza nguvu ya Roho Mtakatifu.
-unaposoma kwa makini biblia utapata ufunuo zaidi juu ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Kanisa la leo linakosa nguvu ya Roho Mtakatifu kwa kushindwa kusoma neno la Mungu kwa makini kila siku.
3.Uwe Mwombaji.
-Unahitaji kuomba wakati wote,hiyo inatakiwa kuwa tabia yako siku zote.
 
Miasha ndani ya Roho Mtakatifu ni kwa kila mwamini!.

No comments:

Post a Comment