''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 25, 2016

UTOAJI NDIO CHANZO CHA KUBARIKIWA

Mhubiri: Mch kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: 2Wakorintho 8:1-7, Kumb 15:10-14
 
Watu wa Makedonia walitoa kwa furaha na sio kwamba walikuwa matajiri bali walitoa kwa moyo na kwa furaha. Walikuwa na kidogo lakini walotoa, kwahiyo kutoka kwao tunajifunza kutoa sio lazima uwe na vingi nyumbani kwako, ukisoma mstari wa pili;
 
"2 maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao."
 
Walikuwa masikini na katika hali ya kujaribiwa lakini wakamtolea Bwana kwa kumaanisha.
 
Kumb 15:10-14, Enzi zile walikuwa wanatoa kwa ajili ya masikini wanatenga hata mashamba kwa ajili ya masikini, je ni mara ngapi umetoa kwa moyo kwa ajili ya masikini?. Unapotoa kwa ajili ya masikini unapata baraka za moja kwa moja kwasababu umetoa. Haya maneno yapo hai mpaka leo ukitoa tegemea baraka zako.

Kwahiyo leo hii nakukumbusha uwe mtoaji, wewe toa tu kwa moyo, na unapotoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu kazi ya Mungu inaenda mbele Zaidi. Unapotoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu, Mungu atakujaza zaidi na Zaidi, usitegemee kujazwa zaidi na zaidi kama wewe sio mtoaji, utapata baraka nyingi za rohoni na mwilini pia.

Kwasababu unamjua Yesu na unajua kwamba unatakiwa utoe Usipotoa unafanya kosa kwasababu umejua moja ya wajibu wako ni kumtolea Mungu kwa moyo kwahiyo usipofanya unafanya makosa.

Fanya utoaji kuwa tabia yako. Kutoa sio kitu cha muda mmoja tu bali ni kitu cha muendelezo, usiseme mimi nilitoa siku flani kwahyo leo sitoi hapo utakosea, utoaji ni kitu cha muendelezo kutoka moyoni. Ukitaka ulinzi na kuepushwa na mambo mengi kuwa mtoaji, mara nyingine Mungu anatuokoa hata bila sisi kujua hata bila kuomba kwasababu tu wewe ni mtoaji, ukiwa mtoaji Mungu analinda mali zako. Kwahiyo mara nyingine unakosa baraka kwasababu hufuati kanuni za kubarikiwa, pia usiwe mtu wa kujijali mwenyewe.

No comments:

Post a Comment