''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, February 5, 2017

UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Matendo 1:4-9

Katika maisha yako ya kiroho ni muhimu sana kuwa na Roho Mtakatifu kwasababu ndio chanzo cha nguvu yetu. Wakati ule Yesu alipokaribia kuwaacha wanafunzi wake, aliwaambia wanafunzi wake wasitoke Yerusalemu mpaka watakapo pokea nguvu ya Roho Mtakatifu. Na baada ya kupokea nguvu ile ya Roho Mtakatifu wakapata ujasiri na nguvu maradufu za kufanya huduma ya kumtangaza Yesu.  Kwahiyo huyu Roho Mtakatifu ni zawadi kutoka kwa Yesu, Yesu hakutuacha upweke akatupa Roho Mtakatifu.

Nguvu ya Roho Mtakatifu ni kubwa sana na inafanya kazi nyingi mno, ndio inayosaidia kufanya huduma yoyote. Hii nguvu ya Roho Mtakatifu ndio chanzo cha uumbaji;

Mwanzo 1:2 " Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji."

Baba, Mwana (Yesu) na Roho Mtakatifu wanafanya kazi pamoja ni nafsi tatu ndani ya kitu kimoja. 

Katika maisha yako kama Mkristo ni lazima uwe na hii nguvu ya Roho Mtakatifu. Bila hii nguvu hutaweza kufanya lolote, na nguvu hii ikipungua ndani mwako au ikiondoka kabisa,moja kwa moja wewe mwenyewe utagundua kama imepungua. 

FAIDA ZA KUWA NA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU
1. Nguvu hii itakuongezea ujasiri wa kuhubiri na kushuhudia. Matendo 4:31 "Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri."

2. Roho Mtakatifu atakuongoza katika kweli yote, Yohana 16:13 "Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake."

3. Nguvu ya Roho Mtakatifu itakusaidia kulijua, kuelewa Neno vizuri na kulifundisha kwa watu wengine kwa usahihi. Matendo 2:42 "Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali." 

No comments:

Post a Comment