''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Saturday, June 10, 2017

NGUVU YA KIBALI CHA MUNGU JUU YAKO

Mhubiri: Mch. Ambele Chapanyota
Maandiko: Luka 1:28-34


Hakuna kitu chochote kinachoweza kuzuia kusudi la Bwana juu yako, haijalishi hali yako iko vipi au uwezo wako ni wa kiasi gani nguvu ya kusudi la Bwana juu yako itawezesha kila kitu. 

Ni kweli Mariam alichokisema kwamba haiwezekani yeye kuchukua mimba na sababu yake ilikuwa ni ya kweli kabisa kwamba hakumjua mume kwahiyo hawezi pata mimba, lakini kwa Yehova vyote vinawezekana! Haijalishi una sababu ngapi za kitu kutowezekana lakini maadamu tu uko upande wa Yehova vyote vinawezekana. Weka sababu zako pembeni alafu tambua uwezo wa kibali cha Bwana. 

Nguvu ya kibali cha Mungu ni kubwa sana kuliko hata silaha zinazo pigana nawe. Hutakiwi kuogopa vita bali tambua wewe kama mtu wa Mungu, kwenye vita ndipo mahali pa kutokea. Daudi alikuwa hajulikani lakini baada ya kumpiga goliati (sawa na vita/vikwazo) akaanza kujulikana na kikamkuza. Vita ulivyonavyo vinakuongeza hatua na hatua.

Ndani ya Mungu hatuishi maisha yetu bali yaliyo juu yetu! kwasababu hatutegemei mazingira, hali inayokuzunguka au chochote bali Yesu tu. Tunaishi kwa mkono wenye Nguvu ya Yehova, sisi ni milki ya Yehova. Ukiokoka tu na kumtegemea Mungu hakuna kitu unachofanya kwa uwezo wako. 

Kibali cha Mungu ni nguvu isiyoweza kuzuilika, Yusufu walimuweka kwenye kisima wakizani ya kuwa atafia hapo lakini badae wakamuuza pia wakazani tena kwamba wamemaliza hatafanikiwa kumbe wanazidi kumsogeza kwenye kusudi la Mungu. No comments:

Post a Comment