''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, June 11, 2017

PAMOJA NA MUNGU UTAVUKA NG'AMBO!

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Yoshua 1:1-9

Wakati huo Musa alikuwa amekufa kwahiyo Joshua akachukua kujiti, haikuwa na namna ilibidi yeye ndiye awaongoze wana wa Israel; na alikuwa haelewi atawaongoza vipi wana wa Israel kwasababu kuwaongoza kundi kubwa vile ilikuwa sio kazi ndogo. Kwahiyo Mungu akawa anamtia moyo Joshua, ni kweli kwamba atakutana na changamoto nyingi lakini awe hodari na moyo wa ushujaa maana yeye ndie atawavusha mto yordan. Katika changamoto zako uwe hodari na moyo wa ushujaa.

Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana."

Utavuka upande wa pili lakini ni lazima umtii Mungu. Mungu yuko tayari kukuvusha ng'ambo ya pili na ana uwezo huo anachohitaji ni wewe kuwa mtii wa Neno lake, kuwa mtii wa mapenzi yake kama Neno lake linavyokuelekeza. 

Yoshua 1:9 "Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako."

Mungu akukuahidi kwamba changamoto hazitakuja, ni kweli changamoto zitakuja lakini amekuhakikishia kuwa pamoja nawe, zinapokuja unatakakiwa uwe hodari na moyo wa ushujaa, usiogope usitetereke Mungu yuko pamoja nawe. Mungu ana njia nyingi zaidi ya jinsi unavyofikiri. Kuwa hodari na moyo ushujaa mwingi. Chukua muda wako mwingi kusoma Neno la Mungu na kumwambia Mungu mahitaji yako. Majaribu yakija jiambie mwenyewe kwamba kwa Jina la Yesu vyote vinawezekana. 

Acha kuyumba yumba acha kuangalia kushoto ama kulia angalia Neno la Mungu linasemaje, tulia kwa Mungu tu, acha kutegemea akili yako au kutegemea wanadamu bali Mungu tu. Hutakufa njiani bali utafika ng'ambo! tenga muda wako mwenyewe kusoma Neno la Mungu (Biblia), kuomba na kutafakari, kutafakari ni kitu cha muhimu, muda wa kimya ukiwa wewe na Mungu ni wa muhimu sana. Ukifanya hivyo kwa uaminifu utashinda jaribu lako kwa ushindi mkuu.

No comments:

Post a Comment