''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, October 15, 2017

UFALME WA MBINGUNI

Mhubiri: Mr. Frank Mwalongo
Maandiko: 2Petro 1:11, Zaburi 10:16, Mathayo 6:31-33, Warumi 14:17

Hapa Duniani kuna falme nyingi lakini ufalme wa Mungu ndio ulio mkuu na unadumu milele yote. Sisi sote kabla hatujaokoka tulikuwa kwenye falme ambazo ni dhaifu sana na zisizodumu, lakini baada ya kumpokea Yesu maishani mwetu tukahamishwa na kuja kwenye ufalme mkuu sana na Mungu aliye hai, unaodumu milele na milele. 

Bwana Yesu alikuja kwetu ili kuleta ufalme wa Mungu. Biblia inasema wokovu si zaidi ya chakula na mavazi, baada tu ya kuokoka unatakiwa kuutafuta ufalme wa Mungu kama ajenda ya kwanza kwenye maisha yako, na mengine ndio yafwatie. Tunapokuwa tunaishi katika maisha haya ya kuokolewa tunatakiwa tujihoji kama bado tupo ndani ya ufalme wa Mungu au tayari tumeshatoka nje ya ufalme wa Mungu. 

Ushindi wetu wa maisha ni katika neno la Mungu, inabidi tuushikilie ufalme wa Mungu kikamilifu zaidi, kuna watu wanaogopa hata kunena mambo ya ufalme wa Mungu. Inabidi ujichunguze maisha yako menyewe.

No comments:

Post a Comment