''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Thursday, October 26, 2017

AMKA NA UWE HODARI!

Mhubiri: Mzee Kiongozi, Elifuraha Mumghamba 
Maandiko: Waamuzi 6:7-27,7:19-22

Gideon aliambiwa kuwa yeye ni hodari, lakini Gideon alikataa akasema yeye ametokea kwenye familia ndogo sana ya Manase kwahoyo akajidharau mwenyewe. Mungu akikuita wewe ni hodari je utakataa? 

Kwenye Waamuzi 6:13 Gidieno akauliza kama Mungu yupo pamoja nao inakuwaje wanateswa sana hivi na ya kwamba Mungu amemuacha huko midiani. Lakini hebu tujiulize hivi ni kweli Mungu aliwaacha au wao ndo walimuacha Mungu??, mara nyingi watu wakimuacha Mungu wanamlalamikia Mungu kwamba wameachwa, Yoshua 1:5 alisema hatatuacha, ukiona huna uwepo wa Mungu ujue wewe ndo umemuacha Mungu au unapita kwenye jaribu anacheki kama uko tayari kufanya kitu kwa ajili yake kama Ibrahimu alivyoambiwa amtoe mtoto wake wa pekee, aliacha mpaka alivyokaribia kumchinja ndipo Mungu akamwambia basi amejua kama anampenda.

Kubali Mungu anachosema, kama Mungu amekwambia wewe ni hodari kubali kwasababu Yeye atakutia nguvu. Yohana 15:5, bila Yesu huwezi kufanya lolote, Yesu Kristonndiyo anayekuwezesha. Ni kweli Gideon alikuwa ametoka kwenye familia iliyo dhahifu lakini kama Mungu amekwambia wewe ni hodari inamaanisha yuko na wewe, na kweli baadaye Gideon alivyokubali kufanya kazi, Mungu alimtumia Gideon kufanya mambo ya ajabu sana. Walivyoenda kwenye vita ni Mungu ndio aliowashindia kwasababu, wao hawakupgana bali walipiga tu tarumbeta na Mungu akafanya wale majeshi yakakimbia.

Kwahiyo mwanzoni Gideon alihitaji uamsho wa kumfanya awe hodari, ndio tangu mwanzoni alikuwa ni hodari lakini alikuwa anajiona kuwa hawezi hafai. Watu sahivi wanasema maisha magumu lakini wewe kama mtu uliokoka hutakiwi kusema hivyo kwasababu Mungu ndio anayekupa. Kuokoka kuna maanisha kuwa na Mungu muda wote hata kama mambo yanabadilika, usikubali kumuacha Mungu wala kukata tamaa. 

No comments:

Post a Comment