''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Tuesday, October 31, 2017

MWITO WA UHUSIANO MZURI

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Mathayo 22:39-40

Uhusiano mzuri msingi wake ni UPENDO. Kama unataka uhusiano mzuri na Mungu, na wa mwenzako ni lazima uwe na upendo, ni lazima umpende Mungu pia na jirani yako. Huwezi kuwa na mahusiano mazuri na Mungu kama hujaamua kumpenda kwa kumaanisha, hivyo hivyo huwezi kuwa na mahusiano mazuri na jirani yako kama humpendi. Mahusiano mazuri yanategemea upendo, bila upendo huwezi kuwa na mahusiano mazuri. 

Kama hutengenezi mahusano mazuri na mwenzako siku ya shida hataweza kukusaidia au atakusaidia kidogo sana. Abraham alikuwa na uhusiano mzuri na Mungu, ndio maana alifanikiwa kwenye mambo yake sana, mfalme Daudi alifanikiwa sana kwasababu ya mahusiano mazuri na Mungu, wote hao walimpenda Mungu kwa kumaanisha. Kwahiyo kama una uhusiano mzuri na Mungu ukiingia kwenye maombi, utapata msaada kwa urahisi zaidi na upesi kuliko mtu ambaye hana uhusiano mzuri na Mungu. 

Muda wa jaribu kama huna mahusano mazuri na Mungu utaomba sana  na kuteseka sana mpaka upate mpenyo, lakini kama una mahusiano mazuri na Mungu, Mungu atakusaidia kwa haraka zaidi. Kwenye 2Wakorintho 10:3-6, vita vyetu sio vya kimwili bali ni vya rohoni sasa utashindaje vita vya rohoni kama huna mahusiano mazuri na Mungu ambaye ni roho, vile vita huwezi kupigana kwa akili zako au nguvu zako, kuna maprofesa wazuri lakini wamefungwa na shetani, unazani utamshindaje shetani bila kuwa na uhusiano mzuri sana na Mungu?.

Ili kutengeneza mahusiano mazuri na Mungu wako, fanya yafuatayo:

1. Kuwa na tabia ya kusoma Biblia, mpe Mungu nafasi ya kwanza
2. Kuwa mwaminifu kwenye kazi yake Mungu, eg. toa fungu la kumi, fanya kazi aliyokupa kwa umakini
3. Tafuta kuelewa kwanini Mungu anafanya kitu flani kwako
4. Kuwa mtu wa amani sana, pia uwe ni mtu wa kusuluhisha wengine
5. Kuwa mtu unayesamehe, kama Yesu alivyosamehe Math 6:14-15
6. Weka moyo wako safi muda wote
7. Wajali wengine kama unavyotamani kujaliwa Matha 7:10
8. Onyesha tabia na mwenendo mzuri 1Kor 5:2, 1Wath 5:22

No comments:

Post a Comment