''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, January 28, 2018

NENO LA MUNGU NDIO KWELI

Mhubiri: Mr. Frank Mwalongo
Neno: Yohana 1:14, 8:32, 16:13-15, 17:13-17, Zaburi 25:4-5

Neno linasema Yesu alijaa na Neema na Kweli, alijaa Kweli kwasababu hapa duniani kulikuwa hakuna Kweli. Hii kweli inayoongelewa hapa ndiyo Mungu mwenyewe, Neno la Mungu ndio Kweli na Kweli ndio Neno la Mungu.

Yohana 8:32 "Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru." Kweli ambayo ni Neno ambayo ni Mungu mwenyewe litakuweka huru. Kweli ilikuja duniani ili kukuweka huru, huru mbali na dhambi, huru mbali na vifungo vya shetani. Yesu alileta Kweli, alitumia muda wake mwingi sana kufundisha hiyo Kweli wakati alipokuwa hapa duniani. tukapata mafundisho mazuri kutoka kwa Yesu. 

Unahitaji sana kuijua Kweli, kwasababu hakuna kingine kinachoweza kukuweka huru zaidi ya Kweli ya Mungu. Ndio utasoma sana shule ili kuondoa ujinga lakini elimu ya hapa duniani haitakuweka huru, elimu ya hapa duniani hubadilika badilika lakini Neno la Mungu halibadiliki na lina nguvu ya kukuweka huru. 

Yohana 16:13-15, Hapa Yesu alikuwa anaongea na wanafunzi wake kabla ya kupaa, haya ni mafundisho ya mwisho ya muhimu kabla hajaondoka na kati ya mambo aliyowaambia ni kuhusu Roho wa Kweli/ Roho Mtakatifu, umuhimu wa Roho wa Kweli. Huwezi kuelewa Neno/ Biblia bila Roho. Ukisoma Biblia bila Roho utaiona ya kawaida tu.

Kuna mambo mengine yanayotokea kwenye maisha yako huwezi kuyaelewa bila msaada wa Roho Mtakatifu; anasema huyo Roho atawafundisha Kweli Yote. Lakini pia Mungu ni mpana sana huwezi kumuelewa Bila msaada wa Roho wa Kweli. Amua kuwa na tabia ya kusoma Neno la Mungu mara kwa mara, ile tabia itakufanya umuelewe Mungu zaidi na zaidi.

Yohana 17:13-17; Kila mara unaposoma Neno unatakaswa na ile Kweli, kila mara unaposoma Biblia kuna kitu kinatokea katika ulimwengu wa roho. Kwahiyo unapoacha kusoma Biblia siku 2 au 7 wiki nzima mpaka jumapili, inamaanisha unakuwa hujatakaswa wiki nzima. 

Sema maneno haya na mimi "Mungu niwezeshe kusoma neno la Mungu kwa bidii kila  siku ninapopata nafasi, nipe muda wa kusoma Biblia".

No comments:

Post a Comment