''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, February 4, 2018

TAKA KUJAZWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU KIKAMILIFU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Matendo 1:4-8

Bila Roho Mtakatifu hatuwezi kufanya kitu na ndio maana Yesu aliwasisitiza sana wanafunzi wake wasitoke Yerusalemu mpaka watakapopata Nguvu hii ya Roho Mtakatifu.

Ili kitu chochote kifanye ni lazima ndani kuwe na nguvu fulani, ili gari lifanye kazi ni lazima kuwe na nguvu ya injini, bila nguvu ya injini gari halina maana, vivyo hivyo Mkristo bila Nguvu ya Roho Mtakatifu huyo sio Mkristo. Ili kuwa Mkristo wa kweli ni lazima uwe umejazwa hii Nguvu za Roho Mtakatifu.

Tafadhali tafadhali jitahidi uwe na hii Nguvu ya Roho Mtakatifu. Kazi yote ya kanisa inategemea hii Nguvu ya Roho Mtakatifu, huwezi kuhudumu bila nguvu ya Roho Mtakatifu. Hii nguvu ya Roho Mtakatifu ukiwa nayo inafanya hata watu wanaokuzunguka kuvutiwa na Yesu uliye naye.  

Tatizo kubwa la sasa watu wengi hawasomi Biblia wanaziweka tu mpaka jumapili, sasa kama kweli unaitaka hii Nguvu ya Roho Mtakatifu ni lazima uwe unasoma Biblia kila siku. Bila kuwa na tabia ya kusoma Neno/ Biblia mara kwa mara Roho Mtakatifu hawezi kukaa ndani mwako kwasababu Roho Mtakatifu anatumia Neno lililo ndani mwako kufanya kazi. Tupo nyakati ambazo kila mtu anasema yuko 'busy' lakini tambua bila Neno huwezi kuwa na Nguvu za Roho Mtakatifu, na bila Nguvu za Roho Mtakatifu kamwe huwezi kuishi maisha matakatifu.

"Efeso 6:10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake."

No comments:

Post a Comment