''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, February 11, 2018

ACHA KUFUATA NAMNA YA DUNIA HII

Mhubiri: Mr. Leandri Kinabo
Maandiko: Waefeso 4:17-24


Paulo ameelezea wazi kabisa kuhusu watu wanaofuata mambo ya dunia na watu watakatifu, kwanzia mstari wa Efeso 4:17-19; "17 Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao; 18 ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao; 19 ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani". Hapa anaelezea sifa za mtu anayeishi kwa kufuata namna ya dunia hii, anaye enenda kama mmataifa ambaye amejaa ubatili ndani mwake.

Na kwanzia Efeso 2:1-3, "Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; 2 ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; 3 ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine."

Bado anaonyesha utofauti  wa mtu mtakatifu na anayefuata namna ya dunia hii, kwamba tulikuwa tumekufa kiroho. Alisema hivi ili kutukumbusha kwamba tuwe makini na hii dunia. Dunia ina mambo mengi sana na sio kila jambo ni zuri kwako wewe kama mtu uliyeokoka. 

Kuwa makini sana na hizi hali mbili ya kuwa mtakatifu na kuwa kama mmataifa kwasababu kama hutakuwa makini unaweza kurudi nyuma na kuanza kufuata mambo ya dunia hii. Kinaacho okoa ni roho yako, na mtu aliyeokoka kweli anajua utofauti wa hizi hali mbili, lakini watu ambao hawajaokoa  huwa hawaelewi utofauti wa hizi hali mbili na huwa wanashangaa kwanini unaacha starehe na kuamua kuokoka. 

Efeso 4:20-24 "Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo; 21 ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu, 22 mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; 23 na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; 24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli."

Tuweke mbali utu wetu wa zamani, yaani usirudie kuwa mtu yule wa zamani, usirudie kufanya mambo uliyokuwa unafanya kabla ya kuokoka wala hata usiyatamani. Ni  lazima ujue jinsi ya kujitenga na mambo ya dunia kwasababu kama utalala usingizi wa kiroho ni lazima utarudi nyuma kiroho. Sisi kama watu wa mbinguni tunakuwa wageni katika hii dunia.

 Galatia 5:16-18 "Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria."

Ni lazima tuishi kwa kuongozwa na Roho, vitu hivi viwili roho na mwili huwa vinashindana kiasi ya kwamba ni lazima uchague kimoja, lakini ukumbuke mwili una asili ya dhambi na sisi kama watu tuliookoka ni lazima tufuate Roho.

No comments:

Post a Comment