''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, February 18, 2018

IMANI YETU INA NGUVU NA NI YA THAMANI

Mhubiri: Mch. Mussa Elias
Maandiko: Marko 2:1-12, Yuda 1:3, 2Petro 1:1

Hii ni stori rahisi sana lakini iliyojaa nguvu nyingi sana, huyu kijana au vijana(hawa vijana wanne) walimbeba mwenzao aliyepoooza ambaye alikuwa amepooza mwili mzima, alikuwa hawezi kufanya chochote. Na waliposikia kwamba Yesu amekuja kwenye mji wao wakatafuta nyumba aliyopo Yesu kwasababu waliamini kwa uhakika kabisa kwamba wakimpeleka mgonjwa wao Yesu atamponya, waliamini kabisa bila mashaka kwamba mwenzao atapona. Na ile imani ndani yao ikawapa ujasiri wa kwenda mpaka kuamua kutoboa dari. Na hapa unagundua sio tu waliompeleka mgonjwa walikuwa na imani bali hata mgonjwa mwenyewe alikuwa na imani ya kwamba Yesu atamponya.

IMANI INAKUJA KWA KUSIKIA, NA UNAPOSIKIA NDIO UNAPOPATA NGUVU NDANI YAKO YA KUFANYA KITU, na kwenye imani kuna wokovu, imani hata siku moja haiwezi kukuangusha. Ndani mwako jenga imani ambayo itakupa nguvu. Mwamini Yesu katika hali yoyote bila kujali hali halisi inayokuzunguka, hata kama unapita hali ngumu kiasi gani weka imani yako kwa Yesu bila kukata tamaa, wale vijana walivyoona watu wengi hawakukata tamaa mpaka wakaamua kutoboa dari. Na usizani kila mtu ataelewa jinsi unavyofanya jambo lako kwa imani, wengine watakuona kama mjinga lakini mwishoni utakapopokea muujiza wako ndipo watakapokuelewa.

Imani ndio kiunganishi kikuu kazi yako wewe na Yesu, bila Yesu huwezi kupokea wokovu, bila kumwamini Yesu huwezi okolewa. Kwahiyo imani yetu ni kwa Yesu tu na sio vinginevyo, wakati wa sasa kumekuwa na dini nyingi zinazodanganya na kufanya watu wamaamini juu ya vitu sana au mtume fulani sna kuliko anavyomwamini Yesu, kuwa makini sana na makanisa kama hayo.


No comments:

Post a Comment