''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, June 3, 2018

MUNGU ANAKUPENDA!

Mhubiri: Mzee Kiongozi, Dr. Mumghamba
Maandiko: Isaya 43:1-6, 1Yohana 3:16, Daniel 10:11, Yoh 13:1, Maombolezo 3:22-23

Katika hali yoyote ile unayopitia hivi sasa, Mungu yupo upande wako. Ukipita kwenye moto hutaungua hutakuwa majivu Mungu atapita na wewe, hatakuacha uangamie kwasababu anakupenda sana. 

Isaya 43: 1-6 "1 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. 2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. 3 Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. 4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. 5 Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi; 6 nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia."

Mungu anasema usiogope  maana kwanza amekukomboa alafu amekuita kwa jina lako , kwasababu wewe u wake, kwahiyo Mungu anakupenda mno. Mungu ndiye aliyekuchagua wewe maana wewe hukustahili upendo wa kiasi kile maana kama wanadamu hatukufanya chochote cha kumfanya Mungu atupende bali ni kwa neema tu anatupenda hivyo. Mungu anatupenda upendo wa agape, upengo wa agape ni ule unaompenda mtu ambaye hata hastahili.

Mungu anakupenda sana lakini ukiangalia si mara zote unampendeza mpaka kwenye Mika 6:3 anakuuliza kwa upole amekufanya nini mpaka umeamua kutokufuata sheria zake, kama Mungu anakupenda kiasi kikubwa hivi kwanini unamtenda dhambi? kwanini unamkosea Mungu? kwanini hufuati maagizo yake?

Mika 6:8, inakuelekeza cha kufanya, kwasababu anakupenda sana unapaswa kujinyenyekesha mbele zake na kufuata maagizo yake. Tambua kuwa Mungu anakupenda sana, ni wajibu wako pia kumpenda Mungu sana na kufuata maagizo yake. Ubarikiwe.

No comments:

Post a Comment