''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, May 28, 2018

JIPANGE BINAFSI KWA AJILI YA INJILI

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Warumi 10:14-15, 2Wakorintho 8:1-7

Wewe ndio mhusika halisi wa injili, Wewe ndio mhusika wa kuwaambia wenye dhambi kuwa Yesu anaokoa, anasamehe dhambi. Kuna njia nyingi za kutekeleza wito huu wa injili; kuna njia ya kwenda mwenyewe kuwashuhudia watu lakini pia kuna njia ya kuwapeleka watu (Wainjilisti) sehemu za mbali wakahubiri injili kwa kutumia pesa yako.


Warumi 10:14-15 "Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!"

Wataendaje pasipo kupelekwa? Peleka injili leo kwa kutumia pesa yako, changia huduma ya injili ili watu waweze kwenda kuhubiri sehemu za mbali. Wewe ni balozi wa Yesu, na kama wewe ni balozo wa Yesu basi unahusika kikamilifu kutangaza habari ya Yesu.

2kor 8:1-7, Watu wa Makedonia walikuwa ni watu wa kawaida sana, sio kwamba walikuwa na hela sana lakini walitoa kwa uaminifu sana zaidi ya ilivyotegemewa. Walimtolea Mungu kwa uaminifu kwa ajili ya injili. Kwanzia leo panga kuwa mtoaji mwaminifu toa sana kwa Mungu, mtoaji hapungukiwi hata siku moja, kama unataka uwe na mafanikio ya kweli mtolee Mungu. Na kama Mungu anakupa pes aalaf UKASHINDWA KUPANGA KIASI KIZURI KWA AJILI YA MUNGU hiyo pesa hutoi hata kdg kwa Mungu san san kweny injli hiyo pesa haitakaa itakuwa kama umeiweka kwenye mvuto wenye matobo, utaaanza kupata mambo ya ovyo ovyo ya kumaliza pesa bila mpango mara mtu flani kaumwa, mara hela inahitajik huku haitakaa

 Ukitoa pesa yako kwaajili ya ajili ya Injili unakuwa hujapoteza bali utapata faida nyingi.  Pesa yako itafanya mtu fulani ampate Yesu na hiyo ni faida kubwa sana. Anza leo kuwekeza kwenye injili uone kama utafilisika!. 

No comments:

Post a Comment